Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Michezo Singida Big Stars yamwita Rais Samia
Michezo

Singida Big Stars yamwita Rais Samia

Spread the love

TIMU ya Singida Fountain Gate, maarufu kama Singida Big Stars, imemwalika Rais Samia Suluhu ahudhurie katika mechi zake  kama anavyofanya kwa timu nyingine kubwa nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida…(endelea).

Mwaliko huo umetolewa jana na Singida Big Stars, wakati wanazungumzia ujio wa Rais Samia mkoani Singida, ambaye anafanya ziara ya kikazi ya siku mbili inayoishia leo tarehe 16 Oktoba 2023.

Mbali na kumuomba Rais Samia ahudhurie katika mechi zake, Msemaji wa Singida Big Stars, Hussein Masanza amesema wanajipanga kushiriki michuano ya kimataifa ili wanufaike na ofa yake ya kupata milioni tano kwa kila goli, aliyoahidi kutoa kwa timu za Tanzania zitakazoshiriki katika michuano hiyo.

“Nilitamani ifike siku ya leo tupate fursa ya kumwalika katika mechiz zetu, tuna mechi nyingi tunazesha tungefurahi kumualika hata Dodoma akipata nafasi aje. Tumezoea kumuona mama yetu akienda mechi za Simba na Yanga, siku moja aje za Singida,” amesema Masanza na kuongeza:

“Tunafahamu mama ni mwanamichezo, hamasa zake tumeziona tungetamani kuwa miongoni mwa wanufaika wa goli la mama sababu tumeshiriki michuano ya kimataifa bahati mbaya tumetolewa Misri, lakini tunajipanga msimu ujao tupate goli la mama.”

Kwa upande wake mchezaji wa timu hiyo, Habib Kyombo, amesema “tumeguswa sana kwa kujitoa kwake michezo yetu na michezo ameweka goli la mama kila timu zinazoshiriki mashindano makubwa , na sisi tunajiandaa vizuri ili msimu ujao tuweze kupata goli la mama.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Beti na Meridianbet mechi za leo

Spread the love IKIWA leo hii ni Jumapili tulivu kabisa, Meridianbet wanamkwambia...

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa tu kutoka Meridianbet

Spread the love  IKIWA leo hii ni Jumamosi nyingine na tulivu kabisa,...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

error: Content is protected !!