Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia aonya chuki, makundi Uchaguzi Serikali za mitaa
Habari za SiasaTangulizi

Samia aonya chuki, makundi Uchaguzi Serikali za mitaa

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania wadumishe amani na upendo kuelekea kipindi cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Rais Samia ametoa wito huo leo tarehe 16 Oktoba 2023, wakati akifungua Daraja la Msingi, lililoko wilayani Mkalama, Mkoa wa Singida.

“Niwaombe kuendelea kutunza amani na utulivu ndani ya nchi yetu, tunaelekea kwenye chaguzi mwakani,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amewataka wananchi kuepusha makundi kuelekea chaguzi zijazo “tujitahidi kuepusha makundi, najua kwenye uchaguzi pia una mkono wa Mungu inawezekana unataka sana kuchukua hiyo nafasi lakini Mungu hakukupangia kuchukua hiyo nafasi.”

“Kwa hiyo unapokosa tusianze kutengeneza makundi tukaanza kubomoa chama chetu tukafanya maendeleo yasipatikane tukaanza kufanya chuki, hapana huko tusifikie niwaombe sana dumisheni umoja wenu upendo na mshikamano tufanye chaguzi zetu vizuri zitupe sura chaguzi unaofuata,”amesema Rais Samia.

Mkuu huyo wa nchi amewataka wananchi kuwachagua viongozi watakaowatumikia.

“Tutakuwa na chaguzi za serikali za mitaa, niwaombe sana ndugu zangu kwenye jambo hili moja kuweka watu watakaowatumikia, msiende kuweka kwa watu watakaopitisha watu wengine, kama mnachagua watu katika uchaguzi ule wekeni watu ambao mnajua watakuja watutumikie wa Mkarama,”amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

error: Content is protected !!