Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kesi mauaji ya wanaharakati wapinga ubaguzi yafufuliwa
Kimataifa

Kesi mauaji ya wanaharakati wapinga ubaguzi yafufuliwa

Spread the love

Wizara ya sheria ya Afrika Kusini inatarajia kufungua tena jalada la uchunguzi wa mauaji ya wanaharakati wanne wapinga ubaguzi moja tukio baya ambalo mashtaka yaka hayajafikia kwa takriban miongo minne. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Wanaharakati hao wanne waliokuwa wanafahamika kwa majina ya Cradock Four walitekwa na kuuawa wakati walipokuwa wakijerea nyumbani eneo la Kusini mwa mji wa Cradock mwezi Juni 1985 baada ya mkutano.

Miili ya wanaharakati hao wanne– Matthew Goniwe, Sparrow Mkonto, Fort Calata na Sicelo Mhlauli—iligundulika baada ya siku kadhaa, ikiwa imeungua vibaya na ikiwa na majeraha ya kuchomwa visu.

Vikosi vya usalama chini ya utawala wa kibaguzi vinashukiwa kuhusika na mauaji hayo. Lakini hakuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua za kisheria.

Waziri wa sheria nchini humo, Ronald Lamola amesema katika taarifa yake jana Ijumaa kuwa ilikuwa “ni haki kwa familia za marehemu ambazo zimekuwa zikisubiri kwa miongo minne kujua ukweli kuhusiana na wahusika wa mauaji ya wapendwa wao.“

Uchunguzi umefanyika mara mbili—mwaka 1987 na 1993—lakini uchunguzi huo ulizua maswali zaidi kuliko majibu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!