Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Biashara Kampuni 500 kushiriki kongamano  kutathmini viwanda nchini
Biashara

Kampuni 500 kushiriki kongamano  kutathmini viwanda nchini

Spread the love

KAMPUNI 500 kutoka China, Tanzania, Angola, Kenya na Ethiopia zinatarajiwa kukutana tarehe 25  Septemba 2023 jijini Dar es Salaam, kutathmini eneo la viwanda na uwekezaji kati ya China na Tanzania. Anaripoti Selemani Msuya…(endelea).

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa SinoTan Industrial Park, Janson Huang wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Amesema kuanzia  tarehe 23 hadi 26 Septemba, ujumbe wa wawakilishi wa kibiashara takribani 126 ukiongozwa na Baraza la Mkoa la Zhejiang nchini China watakuwepo kwa ajili ya kongamano hilo la siku moja.

“Katika uhamasishaji wa biashara ya kimataifa na Serikali ya Watu wa Jinhua italeta wafanyabishara na wawekezaji a Tanzania Septemba 25, mwaka huu ambao watakaa na wenzao wa Tanzania, Kenya, Angola, na Ethiopia kutathmini eneo la viwanda kat ya China na Tanzania chini ya mwongozo wa Ubalozi wa China nchini,” amesema.

Huang amesema katika mkutano huo pia watajadiliana kuhusu uwekezaji wa kati ya nchi hizo ambapo ameweka bayana kuwa kati ya kampuni zaidi ya 100 zinazokuja zipo baadhi zimeonesha nia ya kuwekeza nchini.

Amesema mwamko wa kampuni kutoka China kuja kuwekeza Tanzania unatokana na uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ameuonesha kwa kipindi kifupi tangu aingie madarakani.

Mwenyekiti huyo amesema pia mkutano huo utahusisha watu kutoka serikalini ambao watatumia fursa hiyo kuangalia ni fursa ambazo zinapaswa kupewa kipaumbele.

Huang amesema makampuni yanayokuja kwenye kongamano hilo yanajihusisha katika sekta ya dawa, mashine na vifaa, bidhaa za majumbani za kila siku, huduma za usafirishaji, na nyinginezo.

“Baadhi ya makampuni ndani ya ujumbe wamevutiwa kuwekeza katika maeneo afya, usafi, ulinzi wa mazingira, huduma za usafirishaji, na utengenezaji wa vifaa, lengo likiwa kuanzisha ushirikiano wa muda mrefu na idara za serikali na biashara nchini Tanzania,” amesema.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Ubalozi wa China Yang Zeyu amesema kongamano hilo lenye ajenda viwanda na uwekezaji ni mwendelezo wa nchi yao kushirikiana na Tanzania kukuza uchumi na ushirikiano.

Amesema China itaendelea kushirikiana na taasisi zote ambazo zinaonesha nia ya kuchangia ukuaji wa uchumi na huduma za kijamii.

“Mwaka ujao China na Tanzania zitatimiza miaka 60 ya ushirikiano wa kidiplomasia, hivyo kinachofanywa na kampuni kutoka Zhejiang-Jinhua ni mwendellezo wa mashirikiano mema kati ya nchi hizi mbili na tunaamini wengine wataendelea kuja siku zijazo,” amesema.

Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Uwekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), John Mnali amesema ushiriki wa China kwenye kongamano hilo unaenda kuongeza kasi ya uwekezaji kwenye miradi ya maendeleo hapa nchini.

“Tangu mwaka 1997 hadi 2023 china imewekeza miradi 1,134 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 10.5 na kuajiri Watanzania 136,204, hivyo tunaamini kwamba kongamano hilo linaloshirikisha zaidi ya kampuni 500 litafungua fursa nyingine,” amesema.

Mnali ametoa wito kwa Watanzania kushiriki katika kongamano hilo, ili waweze kujifunza teknolojia na mbinu mbalimbali ambazo zitawezesha kuongeza uwekezaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) Leodgar Tenga, amesema wao kama wadu muhimu katika sekta ya viwanda watatumia kongamano hilo kujifunza mambo mbalimbali ambayo China imepitia hadi kufika hapo walipo.

Amesema China imepiga hatua katika sekta ya viwanda, hivyo wawekezaji wa ndani wanapaswa kujitokeza kwa wingi Septemba 25, ili waweze kubadilisha ujuzi na mawazo.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Biashara Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Kinanasy Seif ametoa wito kwa kampuni za Tanzania kuchangamkia fursa hiyo ambayo Tanzania imepata kwa kushirikiana na China kuandaa kongamano hilo.

“Sekta binafsi inajukumu la kuratibu biashara na uwekezaji, hivyo tunawaomba wadau wote wa sekta ya viwanda kujisajili kushiriki kongamano hilo, ili tuweze kujifunza fursa zilizopo kama teknolojia na biashara,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Mwezi wa kutoboa ni huu, cheza Keno Bonanza utusue Maisha

Spread the love MWEZI wa Oktoba wengi hupenda kuuita mwezi wakutoboa wakiwa...

Biashara

Wataalam Uganda wapewa darasa teknolojia mpya uchimbaji madini katika maonesho Geita

Spread the loveMAONESHO ya Teknolojia ya Madini yamezidi kuwa darasa kwa wadau...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!