Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Tanzania kuiunga mkobo Saudi Arabia Expo 2023
Habari za Siasa

Tanzania kuiunga mkobo Saudi Arabia Expo 2023

Spread the love

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeahidi kuiunga mkono Saudi Arabia kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara mwaka 2030 (EXPO 2030). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ahadi hiyo imetolewa leo Jumatatu na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Samwel Shelukindo alipoelezea yaliyojiri katika mkutano kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na Mjumbe Maalum wa Mfalme wa Saudi Arabia, Ahmed Abdulaziz Qattan uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Balozi Shelukindo amesema katika kikao hicho Rais amemhakikishia mjumbe huyo maalum kuwa Tanzania itashiriki mkutano ya Nchi za Kiarabu na Afrika (Afro Arab Summit) na Mkutano kati ya Saudi Arabia na Nchi za Afrika itakayofanyika Jijini Riyadh mwezi Novemba 2023.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemhakikishia mjumbe huyo Maalum kuwa Tanzania itaiunga mkono Saudi Arabia kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya mwaka 2030 alisema Dkt. Shelukindo.

Balozi Shelukindo pia aliongeza kuwa Rais Samia amemhakikishia mjumbe huyo kuwa Tanzania itashiriki Mkutano kati ya Nchi za Kiarabu na Afrika (Afro Arab Summit) na Mkutano kati ya Saudi Arabia na Nchi za Afrika inayotarajiwa kufanyika Jijini Riyadh, Saudi Arabia mwezi Novemba 2023.


Naye Mjumbe Maalum wa Mfalme wa Saudi Arabia, Ahmed Abdulaziz Qattan amesema Saudi Arabia inaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kukubali kuiunga mkono kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya mwaka 2030 (EXPO 2030)

“Kwa niaba ya Serikali ya Saudi Arabia tunaishukuru sana Serikali ya Tanzania kwa kuahidi kutuunga mkono kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya mwaka 2030 (EXPO 2030),” alisema Qattan.

Aliongeza kuwa Saudi Arabia inamshukuru  Rais Samia kwa kitendo cha kukubali Tanzania ishiriki katika Mikutano kati ya Nchi za Kiarabu na Afrika (Afro Arab Summit) na Mkutano kati ya Saudi Arabia na Nchi za Afrika itakayofanyika Jijini Riyadh mwezi Novemba 2023

“Kwa niaba ya Serikali ya Saudi Arabia namshukuru Mheshimwa Rais kwa kukubali kutuunga mkono kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya EXPO 2030 na kukubali kushiriki mikutano kati ya Nchi za Kiarabu na Afrika (Afro Arab Summit) na Mkutano kati ya Saudi Arabia na Nchi za Afrika itakayofanyika Jijini Riyadh mwezi Novemba 2023,” aliongeza Qattan.

Amesema katika kikao hicho wamejadili pia masuala mbalimbali yanayolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Saudi Arabia na Tanzania katika nyanja mbalimbali.

Tanzania na Saudi Arabi zimekuwa na uhusiano mzuri na zimekuwa zikishirikiana katika sekta mbalimbali hususan utalii, biashara za bidhaa za nyama, matunda na mazao mengine ya chakula.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!