WAOMBOLEZAJI wamepanga mistari kwenye barabara za mji mkuu wa Japan – Tokyo kumuaga aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo aliyeuawa Shinzo Abe. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea).
Gari lililobeba mwili wake lilipitishwa katika maeneo muhimu ya kisiasa baada ya kufanyika ibada ya faragha. Hafla hiyo ilifanywa katika hekalu la Zojoji mjini Tokyo na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wa karibu.
Pia mwili wake ulipitishwa katika majengo ya bunge, ofisi ya waziri mkuu na makao makuu ya chama chake cha Liberal Democratic.
Waziri mkuu huyo wa zamani aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi nchini humo, aliuawa kwa risasi Ijumaa tarehe 8 Julai, 2022 wakati akifanya kampeni katika mji wa magharibi wa Nara. Tukio hilo liliishtua Japan na kulaaniwa na jamii ya kimataifa.
Mshukiwa wa mauaji hayi, Tetsuya Yamagami mwenye umri wa miaka 41, yuko kizuizini na amewaambia polisi alimlenga Abe kwa sababu aliamini mwanasiasa huyo alikuwa na mafungamano na kundi moja alilolichukia.
Leave a comment