Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bilioni 570 kunufaisha wanafunzi 205,000
Habari Mchanganyiko

Bilioni 570 kunufaisha wanafunzi 205,000

Spread the love

SERIKALI imesema katika mwaka fedha 2022/2023 itoa Sh. bilioni 573 kwa wanafunzi 205,000 wa elimu ya juu.

Aidha Wizara hiyo imeunda timu ya watu watatu ambao watapotia mchakato wote wa waombaji mikopo nchini. Anaripoti Selemani Msuya … (endelea).

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda leo tarehe 12 Julai, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa Uombaji Mkopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu.

Waziri Mkenda amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imedhmiria kuwapatia mikopo wanafunzi wote wenye sifa, kuwataka wanafunzi ambao wanatarajia kujiunga na elimu ya juu kufuata taratibu zote ili waweze kupata haki hiyo.

Amesema kwa mwaka 2021/2022 Serikali iliipatia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania ( HESLB), Sh.bilioni 570 ambapo wanafunzi 177,800 walinufaika.

Waziri huyo alisema katika msimu huu wa 2022/2023 wanafunzi 205,000 watanufaika na Sh.bilioni 573 zilizopelekwa HESLB, huku Sh.bilioni 3 ikitolewa kama ruzuku kwa wanafunzi 500 wa masomo ya sayansi.

“Tumezindua Mwongozo wa Uomboji Mkopo naamini wahusika watautumia vizuri kuhakikisha wanapata mikopo kwa wakati ili wanapojiunga na vyuo wasipate usumbufu,

Serikali imejipanga kuwapatia wanafunzi wote ambao watakuwa wamekidhi vigezo ambavyo vinahitajika,” amesema.

Amesema hakuna mwanafunzi ambaye atakidhi vigezo atakosa mkopo, hivyo akaitaka bodi hiyo kuhakikisha wanafunzi wanasaidiwa pale ambapo watahitaji msaada.

Profesa Mkenda amesema Serikali itatoa ruzuku kwa wanafunzi waliofaulu vizuri katika masomo ya sayansi ambao watasomea sayansi, uhandisi na elimu tiba.

Waziri Mkenda amesema pia katika mwaka wa masomo 2022/2023 watatoa kipaumbele cha mikopo wanafunzi wa masomo ya kiswahili, ukalimani na lugha nyingine.

Amesema masomo hayo kwa sasa uhitaji wake ni mkubwa duniani hivyo Serikali imeona kuweka mkazo katika kuwaandaa  watalaam.

Aidha, amesema HESLB imeweza kuvuka lengo la ukusanyaji madeni ya wadaiwa wa mikopo ambapo mwaka 2021/2022 wamefanikiwa kukusanya Sh.bilioni 183.8 katika lengo la kukusanya Sh.bilioni 183.

Waziri Mkenda amesema makusanyo hayo ya madeni ni sawa na asilimia 32.2 ya fedha iliyotolewa na Serikali, hivyo kuitaka bodi kuongeza juhudi katika ukusanyaji mikopo.

Pia Waziri amewataka wazazi walioajiriwa wakitaka mkopo wa kusoma au kusomesha watoto wao waende Benki ya NMB ambao wametenga sh.bilioni 200 kwa ajili ya elimu.

Amesema pia benki hiyo imepanga kutoa ruzuku na laptop kwa wanafunzi 100 wenye mahitaji ili waweze kupata elimu ya juu.

“Pia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimetenga fedha za ndani ambazo zitafadhili wanafunzi 50 watakaofanya fanya vizuri katika masomo ya sayansi. Pia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), imetengewa Sh.bilioni 8 kwa ajili ya wanafunzi wanaotoka familia maskini,” amesema.

Mkenda ameitaka bodi hiyo kuzingatia vigezoambavyo wamejiwekea kuhakikisha kila anayestahili anapata haki yake.

Akizungumzia muongozo  wa utoaji mkopo mwaka 2022/2023 amesema Juni 12 hadi 18 utawekwa kwenye tovuti ya bodi kwa lugha ya kiswahili na kiingereza.

Aidha, Waziri Mkenda amesema katika kutatua changamoto za uombaji mkopo wameunda timu ya wataalam watatu ambao watapitia mfumo mzima wa ugawaji wa mikopo kuanzia nyuma hadi sasa.

Amesema timu hiyo itaangalia takwimu za miaka mitano iliyopita itapitia taarifa zote na kuziwakilisha kwenye menejimenti ya Wizara kwa hatua zaidi.

“Tumeunda timu ya watu watatu ambao ni Profesa Allen Mushi, Iddi Makame na Dk.Martin Chegeni.Hawa ni wataalam wa takwimu na mifumo naamini watakuja na ushauri mzuri, amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo, Profesa Hamisi Dihenga amesema bodi hiyo imejipanga kuhakikisha changamoto zinazotokea wakati wa kuomba na kutoa na mikopo.

Profesa Dihenga amesema kila mwanafunzi ambaye atahitajika kupata mkopo atapatiwa iwapo atakidhi vigezo.

Naye Posta Masta Mkuu Maurice Mbodo, Mkurugenzi wa RITA Angela Antony na Mkurugenzi Mkuu wa TASAF Ladslaus Mwanga wamesema watashirikia na  HESLB kuhakikisha wanafunzi wanaoingia chuo kikuu wanajisajili bila usumbufu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!