WATU watano wa familia moja wamefariki dunia katika ajali iliyosababisha vifo vya watu wanane baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso katika barabara kuu ya kutoka Lusahunga kwenda Nyakahura wilayani Biharamulo Mkoa wa Kagera. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kagera … (endelea).
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale, ajali hiyo imetokea usiku wa leo Jumanne tarehe 12 Julai, 2022 ikihusisha gari aina ya Mercedez Benz na lori aina ya Toyota Probox.
Kamanda Mwampaghale ametaja ndugu wa familia moja waliofariki kuwa ni Jesca Ntahimula (45), Magreth Kimuna (14), Adidas Sekanabo (12), Zabloni (6) na Vedastina Sekanabo (8) wakazi wa Nyamalagala.
Wengine waliofariki kwenye ajali hiyo ni dereva wa Mercedes Benz, Vicent Gakuba (52) raia wa Rwanda, mkazi wa Nyamata Rugesela EAST Province, Nyawenda Bisalo (35) na Majaliwa Maige (32), wakazi wa Kikoma.
Kamanda huyo amesemaMiili ya marehemu hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Kituo cha Afya Nyakanazi.
Kamanda huyo amesema uchunguzi wa awlai umebainia chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dreva wa lori aliyehama kutoka upande wake na kuendesha gari upande ambao sio wake kitendo kilichosababisha kugongana uso kwa uso kwa magari hayo.
Amesema dreva wa lori, Vicent Gakuba alitoroka baada ya ajali hiyo lakini polisi walifanikiwa kumkamata baada ya muda mfupi eneo la Rusumo akijaribu kutoroka kwenda Rwanda kwa kutumia lori.
Leave a comment