Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Gavana wa benki kuu Burundi akamatwa kwa ufisadi
Kimataifa

Gavana wa benki kuu Burundi akamatwa kwa ufisadi

Spread the love

DIEUDONNÉ Murengerantwari anatuhumiwa na wizara ya sheria ya Burundi kwa madai ya kuhujumu utendaji wa uchumi wa taifa, ufisadi na ufujaji wa mali ya umma. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea)

Licha ya tuhuma hizo, kiongozi huyo wa zamani hajajibu madai hayo.

Siku ya Jumapili, Rais wa Burundi, Évariste Ndayishimiye alimfuta kazi Murengerantwari na nafasi yake kuchukuliwa na Édouard Normand Bigendako.

Murengerantwari alikuwa ameteuliwa kuongoza benki kuu ya Burundi kwa miaka mitano kuanzia Agosti mwaka jana.

Kwa mujibu wa mwanasheria mkuu wa Burundi, Leonard Manirakiza uchunguzi zaidi kuhusu madai hayo ya ufisadi dhidi ya kiongozi huyo unaendelea.

Aidha, taarifa ya mwanasheria huyo mkuu wa Burundi inasema gavana huyo wa zamani wa benki kuu kwa sasa anashughulikiwa kwa mujibu wa sheria wakati akiendelea kuzuiliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!