Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa El Chapo aomba kurejeshwa Mexico
Kimataifa

El Chapo aomba kurejeshwa Mexico

Joaquin ‘El Chapo’ Guzman
Spread the love

 

RAIS wa Mexico, Andres Manuel Lopez Obrador amesema atazingatia ombi la mlanguzi wa dawa za kulevya Joaquin ‘El Chapo’ Guzman, anayetumikia kifungo kurejea Mexico kutoka Marekani kumalizia kifungo chake kwa misingi ya kibinadamu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mwanzilishi wa genge la ulanguzi la Sinaloa ameomba msaada kwa Rais Obrador, kutokana na madai ya mateso ya kisaikolojia ambayo Guzman, anasema anateseka katika gereza la Marekani.

Rais Obrado aliwaambia wanahabari kwamba wanapitia maombi ya El Chapo. Haikuwa wazi kama Mexico ilikuwa na uwezo wa kukubaliana na ombi hilo.

Mwaka 2019, Mahakama ya serikali kuu mjini Brooklyn nchini Marekani ilimhukumu kifungo cha maisha jela El Chapo baada ya kupatikana na hatia ya kufanya biashara hiyo haramu iliyosababisha vifo vya watu wengi na kuingiza nchini Marekani tani nyingi za dawa ya kulevya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Papa Francis kukutana na wahanga wa vita Sudan Kusini

Spread the love  KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo Jumamosi...

Kimataifa

Polisi ahukumiwa kifo kwa kumuua wakili

Spread the love  MAHAKAMA kuu nchini Kenya imemhukumu kifo Ofisa wa Polisi,...

Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the loveHOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha...

Kimataifa

Papa Francis ayataka mataifa ya nje kuacha kupora mali DRC

Spread the love  KIONGOZI wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya...

error: Content is protected !!