Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu ampa kibarua Rais Samia, aanika atakachoanza nacho akiwasili
Habari za SiasaTangulizi

Lissu ampa kibarua Rais Samia, aanika atakachoanza nacho akiwasili

Spread the love

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, Tundu Lissu, amesema usalama wake pindi atakaporejea Tanzania akitokea nchini Ubelgiji, utakuwa mikononi mwa Rais Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Lissu ametoa kauli hiyo jana jioni, katika mahojiano yake na Sauti ya Amerika (VOA Swahili), alipoulizwa kipi kilichobadili msimamo wake wa kurudi nchini alikokimbia kwa madai ya kuhofia usalama wake.

“Nafahamu kwamba wale waliojaribu kuniua 2017 hawajachunguzwa na hawajakamatwa na watu wanaona kuna vitisho vinajitokeza kwa baadhi ya askari polisi, hiyo haitanizuia mimi kurudi nyumbani. Narudi nyumbani usalama wangu utakuwa kwenye mikono ya Rais Samia na Serikali yake waliotangaza nirudi nitakuwa salama,” alisema Lissu.

Katika hatua nyingine, Lissu alitaja kitu cha kwanza atakachokifanya akirejea Tanzania, Jumatano ijayo tarehe 25 Januari 2023, akisema itakuwa na mkutano wa hadhara, ingawa hajaweka wazi mkutano huo utafanyika wapi.

“Nitakapofika nyumbani siku ya Jumatano naenda kwenye mkutano wa hadhara ambao umeandaliwa na chama changu kama sehemu ya mapokezi yangu. Tunaanza shughuli moja kwa moja, nichukue nafasi hii kuwakaribisha wananchi wanaoweza kuhudhuria mapokezi na mkutano wa hadhara,” alisema Lissu.

Mwanasiasa huyo aliyekuwa mgombea wa Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu uliopita, aliondoka Tanzania kwenda Ubelgiji tarehe 10 Novemba 2020, kwa madai kwamba anakwenda ugahibuni kunusu maisha yake kufuatia vitisho vya kiusalama vilivyoibuka baada ya uchaguzi huo kumalizika.

Hata hivyo, mara kadhaa Serikali ya Tanzania imetoa wito kwa wanasiasa waliokimbia nchi kurejea huku ikiwahakikishia usalama wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

error: Content is protected !!