Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko DC Dodoma awataka Watanzania kutumia gesi badala ya mkaa
Habari Mchanganyiko

DC Dodoma awataka Watanzania kutumia gesi badala ya mkaa

Spread the love

WATANZANIA wameshauriwa kuwa na utamaduni wa kutumia gesi kwa matumizi ya kawaida ili kuepukana na matumizi ya mkaa ambao ni chanzo cha uharibifu wa misitu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma… (endelea).

Ushauri huo umetolewa leo tarehe 29 Julai 2023 na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabiri Shekimweli alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Kikuyu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya usafi wa mazingira ya kila mwisho wa mwezi.

Shekimweli amesema kutokana na kuwepo kwa uharibifu wa mazingira kuna kila sababu ya kuanza kubadilisha mwelekeo wa matumizi ya nishati ya kupitia na kutumia gesi ili kuachana na mkaa.

Mbunge wa Dodoma na Waziri wa Kilimo, Antony Mavunde akishiriki kupanda miti katika kata ya Kikuyu Kaskazini Jijini Dodoma wakati wa kilele cha usafi wa mazingira.

“Kama mnavyojua kwa sasa Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwepo kwa kikomo cha matumizi ya nishati ya mkaa, ikiwa ni njia mojawapo ya kupambana na kutunza mazingira.

“Nataka kuwauliza wananchi wa kata ya Kikuyu, je, ni nani ambaye hana namba ya muuza mkaa? …nataka kuwaambia kuwa kama wananchi mtagoma kununua mkaa ni wazi kuwa biashara ya mkaa itakoma kabisa.

“Kama akina baba wataacha kuwanunua akina dada poa ni wazi kuwa akuna dada atakayefikiria kufanya biashara ya kujiuza na kama vijana wataacha kuvuta bangi hakuna muuzaji atakayeuza bangi hivyo tukiacha kununua au kutumia mkaa basi wakata mkaa na wauza mkaa watajikuta wakiachana na biashara hiyo,” amesema Shekimweli.

Akizungumzia suala la ukataji wa miti Shekimweli amesema kitendo cha kukata miti ovyo ni sawa na kuwa na mgonjwa katika chumba cha watu wahututi waliowekewa mipira ya kupumulia lakini mtu anaunyofoa mpira huo na kusababisha umauti.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo, Antony Mavunde amesema kuna kila sababu ya kutunza mazingira kwa kupanda miti kila kona kwa ajili ya utunzaji wa mazingira kwa faida ya hali ya hewa ya nchi.

Aidha, Mavunde amesema kuna kila sababu ya kupanda miti katika sehemu za taasisi kwa kuwa maeneo hayo ya umma yalikuwa yameachwa nyuma kidogo.

“Nataka kuwaeleza kuwa hii zahanati ya Kikuyu Kaskazini ni lazima iwe sehemu ya mfano kwa utunzaji wa mazingira na ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu wodi ya akina mama kujifungulia itakuwa imeaza kutumika,” ameeleza Mavunde.

Mavunde ambaye ni mbunge wa Dodoma amesema pamoja na mambo mengine amewasihi wakazi wa mkoa wa Dodoma na nchi kwa ujumla kuhakikisha wanatunza mazingira kwa kupanda miti kwa wingi pamoja na kuhakikisha majengo ya umma yanakuwa ya mfano katika kupambana katika utunza mazingira.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari Mchanganyiko

Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio

Spread the loveMRADI wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambao Makamu wa Rais, Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

error: Content is protected !!