Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu: Katiba mpya muarobaini kudhibiti wizi
Habari za SiasaTangulizi

Lissu: Katiba mpya muarobaini kudhibiti wizi

Spread the love

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, amesema Katiba mpya ndio njia pekee ya kudhibiti ‘wizi’ unaotendeka kila awamu ya utawala unapoingia madarakani. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumza katika Mkutano wao uliofanyika leo tarehe 28 Julai 2023 Bukoba mkoani Kagera, Lissu amesema enzi za utawala wa Rais Benjamini Mkapa na Jakaya Kikwete kulifanyika matukio ya uhalifu ambayo hadi sasa hayajachukuliwa hatua.

Amesema kwa kuwa Katiba iliyopo sasa inawalinda viongozi waliopo madarakani hata kama wakifanya makosa ni vema kuwepo na mabadiliko ya Katiba ambayo haitawalinda viongozi pindi watakapotoka au kuwa madaralani.

Amesema katiba hiyo italinda rasilimali za Tanzania bila kujali kiongozi aliyepo madarakani ni wa CCM au lah kwani kila mtu ni binadamu ma chochote kinaweza kutokea.

Aidha, ametoa mfano namna Rais Mkapa alivyoeleza kwenye kitabu chake makosa aliyoyafanya katika ubinafsishaji wa mashirika ya umma lakini hakuna hatua alizochukuliwa.

“Tuyazungumze haya majimboni kwetu na tujipange kulinda vya kwetu, kwa sababu mimi nilimsema Rais Mkapa kwa wizi wake na akanikamata na kukaa na kesi miaka sita ingawa Mkapa alikuwa mkatoliki kama mimi lakini yeye alikuwa mwizi japo alitembea na limsalaba lake.

“Sio Mkapa tu, hata huyu naye ni wale wale wezi walioibia nchi yetu na  Tegeta Escrow bila kusahau maujambazi mengine aliyofanya katika kipindi cha utawala wake na maujambazi mengine ambapo nilipomsema alinifungulia kesi tatu,” amesema Lissu.

Aidha, akizungumzia kuhusu mkataba wa uwekezaji bandari, Lissu alieleza kushangaa namna viongozi wa CCM wanavyozunguka nchi nzima kuutetea mkataba huo ulioingiwa Oktoba mwaka jana kati ya Serikali Tanzania na Dubai.

Amesisitiza kuwa mkataba huo hauna faida kwa Tanzania huku upande wa Serikali ulitaja baadhi ya faida hizo kuwa ni pamoja na ongezeko la mapato pamoja na ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!