Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Tani 13 za dawa za kulevya za kamatwa na watuhumiwa 4,983 hapa nchini
Habari Mchanganyiko

Tani 13 za dawa za kulevya za kamatwa na watuhumiwa 4,983 hapa nchini

Spread the love

 

JESHI la Polisi kupitia kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania limefanikiwa kukamata tani 13 .717 za dawa za kulevya pamoja na watuhumiwa 4,987 katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Jeshi la Polisi Dar es Salaam … (endelea).

Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP. Amon Kakwale amesema katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni 2023, ambapo kitengo hicho cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya kilifanikiwa kukamata kiasi cha kilogramu 9,358.77 sawa na tani 9.36 za dawa za kulevya aina ya bangi.

Ameongeza kuwa tani 4.357 za mirungi, kilogramu 1.86 za heroin pamoja na gramu 220.05 za cocaine zilikamatwa na ekari 105.25 za mashamba ya bangi na mirungi yaliteketezwa.

Katika hatua nyingine ACP Kakwale amesema operesheni hiyo ilifanikiwa kukamata watuhumiwa 4,983 ambapo kesi 3,784 zilifunguliwa na kesi hizo zipo katika hatua mbalimbali Mahakamani.

Mkuu huyo ametoa onyo kali kwa wanaoendelea kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kuacha mara moja kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wakijihusisha na vitendo hivyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Taifa Gas waanika mikakati kupunguza gharama za gesi ya kupikia

Spread the loveKATIKA kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kuhamasisha...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Uingereza yamwaga bil. 9 kumuunga mkono Samia matumizi nishati

Spread the loveWaziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani...

Habari MchanganyikoTangulizi

TMA yatoa taarifa ya uwepo wa Kimbunga “Ialy”

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa ya...

Habari Mchanganyiko

DAWASA yamaliza kero ya maji Nyakahamba iliyodumu kwa miaka 5

Spread the loveMamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Dar es...

error: Content is protected !!