Saturday , 30 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Askofu aonya Watanzania kufanya kazi badala ya kutegemea misaada
Habari Mchanganyiko

Askofu aonya Watanzania kufanya kazi badala ya kutegemea misaada

Askofu Dk. Benson Rutta
Spread the love

ASKOFU Mkuu wa kanisa la Glory to God Ministry for All Nations lenye makao makuu Mailimbili Jijini Dodoma, Dk. Benson Rutta amewataka watanzania kuhakikisha wanalinda amani pamoja na kujibidisha katika kufanya kazi badala ya kutegemea misaada. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza na waumini wa kanisa hilo leo tarehe 9 Septemba 2023 katika ibada maalumu ya kuliombea Taifa.

Askofu mkuu huyo amesema watanzania wana kila sababu ya kuhakikisha wanailinda amani ya nchi pamoja na kuhakisha wanafanya kazi kwa nia ya kujipatia kipato badala ya kuendelea kutegemea misaada.

Katika hatua nyingine kiongozi huyo wa kiroho amesema ili nchi iendelee kuwa na ustawi ni lazima rasilimali za nchi zilindwe kwa nia ya kuendeleza kizazi kijacho.

Kiongozi huyo amesema ili nchi iwe na maendeleo inatakiwa kuwa na watu ambao wana hofu ya Mungu kwa kuhakikisha wanasimamia haki pamoja na kulinda rasilimali za taifa bila kujinufaisha wao wenyewe.

Askofu Dk.Rutta ambaye alikuwa ni kiongozi katika kanisa la Full Gospel Bible Fellowship linaloongozwa na askofu mkuu Zacharia Kakobe na kujiengua kisha kuanzisha huduma yake inayojulikana kwa jina la Glory to God Ministry for All Nations, amesema kazi kubwa ya watumishi wa Mungu ni kuhakikisha wanasimamia ukweli ambao utalifanya taifa kuwa na neema wala siyo hiana.

Mbali na hilo Askofu Rutta amesema ili taifa liwe na ustawi linatakiwa kuwa na watu wenye hofu ya Mungu kwa kusimamia haki na wajibu pamoja na kutopenda kuwaonea watu wanaosimamia ukweli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!