Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Michezo Taifa Stars yatua salama, yapokelewa kwa shangwe na mashabiki
Michezo

Taifa Stars yatua salama, yapokelewa kwa shangwe na mashabiki

Spread the love

TIMU ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) imetua salama alfajiri ya leo tarehe 9 Septemba 2023 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea nchini Algeria kwenye mchezo wa kufuzu mashindano ya AFCON 2023 yatakayochezwa mapema mwakani 2024 nchini Ivory Coast. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Katika mchezo huo uliochezwa tarehe 7 Septemba 2023, Tanzania na Algeria zilitoka zilitoka sare ya bila kufungana (0-0), matokeo ambayo yanazifanya timu hizo kufuzu michuano hiyo, huku Tanzania ikifuzu kwa mara ya tatu katika historia ya mashindano hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutua jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu ambaye aliongoza msafara wa timu hiyo kwa niaba ya Serikali, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa maono yake kwenye sekta ya michezo, hamasa pamoja na kuunga mkono timu hiyo.

Aidha, amewashukuru Watanzania wote kwa sala, dua na maombi yao na kuiunga mkono timu yao ya Taifa na kusisitiza kutakuwa na utaratibu mzuri kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) hatua itakayowezesha mashabiki waende kwa wingi nchini Ivory Coast mwakani 2024 kwenye michuano hiyo ili kuendelea kupeperusha vyema bendera ya taifa.

“Wizara yetu ambayo inaongozwa na Waziri Dk. Damas Ndumbaro itaendelea kuyaishi maono ya rais katika kuiendeleza wa timu ya Taifa na sasa ufadhili na uangalizi utaongezeka zaidi ili Ivory Coast tukafanye vizuri zaidi” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Meridianbet yaibukia Tandika, yafungua duka jipya

Spread the love BAADA ya kupita maeneo mbalimbali hatimae kampuni yaMeridianbet imeibukia...

BiasharaMichezo

Ukiwa na Meridianbet ni rahisi kuwa milionea

Spread the love  CARABAO Cup raundi ya 3 Uingereza inaendelea na mechi...

Michezo

Jezi ya Samatta iliyoifunga Liverpool kuuzwa Genk

Spread the love  KLABU ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji imeamua kuanza...

BiasharaMichezo

Hii ndio historia ya El-Clasico, derby bora zaidi duniani

Spread the love  KILA nchi ina vilabu viwili hasimu na pinzani nje...

error: Content is protected !!