WAKALA wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA), umesema uzalishaji mbegu imeongezeka kutoka tani 500 hadi kufikia 3,500. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tabora…(endelea).
Ongezeko hilo limetajwa leo Jumatano na Mtendaji Mkuu wa ASA Dk. Sophia Kashenge, akizungumza uwekezaji katika sekta hiyo uliofanywa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, tangu alivyoingia madarakani miaka miwili na nusu iliyopita.
“Tunampongeza sana Rais Samia kwa kuongeza bajeti ya ASA iliyotuwezesha kuongeza uzalishaji mbegu kwa kiasi kikubwa,” amesema Dk. Kashenge.
Dk. Kashenge amesema ongezeko hilo linawasaidia wakulima Kupata mbegu bora kwa bei nafuu na kwa uhakika.
Amesema idadi ya mashamba ya ASA imeongezeka kutoka nane hadi 16, yaliyoko Tanzania Bara, ambayo kwa sasa yanayotumika ni asilimia 90.
Dk. Kashenge amesema uwekezaji wa miundombinu Katima shamba la mbegu lililoko eneo la Kilimo, wilayani Nzega, Mkoa wa Tabora, utazalisha mbegu mara mbili mwaka ujao.
Leave a comment