Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Uingereza yatahadharisha raia wake Uganda
Kimataifa

Uingereza yatahadharisha raia wake Uganda

Spread the love

Serikali ya Uingereza imetoa tahadhari kwa raia wake wajiepushe kuitembelea mbuga mashuhuri ya wanyama nchini Uganda ambako watalii wawili, akiwemo raia mmoja wa Uingereza, wameuawa. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Maafisa wa polisi na wa mbuga ya wanyama wamesema watu hao watatu walishambuliwa jana Jumanne na watu waliokuwa na bunduki wakati walipokuwa wakifanya safari katika mbuga ya kitaifa ya Malkia Elizabeth kusini magharibi mwa Uganda na gari yao kutiwa moto.

Shirika la Huduma za Wanyamapori la Uganda limewatambua wahanga wengine wawili kama mtalii wa Afrika Kusini na muongozaji safari wa Uganda.

Polisi wamelinyooshea kidole cha lawama kundi la Allied Democratic Forces (ADF) kwa shambulizi hilo.

Msemaji wa polisi, Fred Enanga amesema vikosi vyao vya pamoja vilichukua hatua mara tu baada ya kupokea taarifa na wanawasaka washukiwa waasi wa kundi la ADF.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!