SERIKALI ya Zanzibar, imetangaza mpango wake wa kufuta mitihani ya darasa la nne kwa shule za msingi na kidato cha pili kwa sekondari, ili kukidhi matakwa ya sera mpya ya elimu visiwani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).
Mageuzi hayo ya elimu yametangazwa leo tarehe 18 Oktoba 2023 na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Mohammed Musa, Zanzibar.
“Serikali itaondoa mitihani hiyo, imeamua kufuta hii mitihani kwanza sio kwamba inafanya mwanafubzi whitinu au inamfanya asiendelee kusoma. Lengo la mitihani ni kumpima kafaulu au hakufaulu, tutaandaa utaratibu mzuri,” amesema Lela.
Leave a comment