IDADI ya maiti zilizofukuliwa na polisi nchini Kenya zimefikia 73. Watu hao waliofunga hadi kufa walikuwa wafuasi wa Kanisa la Good News International jamii moja ya kikristo lililopo katika Kaunti ya Klilifi nchini humo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Maiti hizo zimefukuliwa kwenye makaburi ya jumuiya yaliyopo msituni wa Shakahola uliokuwa unamilikiwa na mchungaji wa kanisa hilo Paul Mackenzie.
Mkuu wa upelelezi wa kaunti ya Kilifi, mashariki ya Kenya, Charles Kamau amethibitisha idadi hiyo na ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba watu wengine watatu wamekamatwa.
Shirika la msalaba mwekundu la nchini Kenya limesema watu 112 hawajulikani walipo.
Rais William Ruto amesema kiongozi wa jamii hiyo ya kikristo ni mhalifu mkubwa.
Paul Mackenzie alikamatwa takriban wiki mbili zilizopita baada ya fununu juu ya kuwepo kwa makaburi yaliyokuwa na maiti 31 za wafuasi wake.
Wafuasi wa kanisa la Good News International walikuwa wanaishi kwa kujitenga kwenye eneo la ekari 800 za msitu wa Shakahola nchini Kenya.
Inatuhumiwa kwamba waliagizwa kufunga mpaka kufa ili kuweza kukutana na Yesu.
Idara ya upelelezi ya nchini Kenya imesema watu 33 wameshaokolewa hadi sasa.
VIONGOZI WANAOONGOZA KUKOSOA MAAMUZI YA VIONGOZI WENZAO TANZANIA….. KWA MBINU ZOTE TULIZANI HUWA MANAKUBALIANA
Mwanasiasa maarufu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche ametema cheche kuhusu sakata linaloendelea la Kampuni ya Twiga Cement kutaka kuinunua Kampuni ya Tanga Cement.
Her Excel. Samia Suluhu
Mr. Daniel Chongolo
Mr. Professor Ibrahim Haruna
Mr. Hamad Masoud Hamad
Mr. Freeman Aikael Mbowe
Mr. John John Mnyika