Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kimbunga Freddy chaua 100 Malawi, Msumbiji
Kimataifa

Kimbunga Freddy chaua 100 Malawi, Msumbiji

Moja ya athari zilizotokea kutokana na KImbunga Freddy
Spread the love

 

KIMBUNGA Freddy, kilichoambatana na upepo mkali na mvua kubwa, kimerejea kusini mwa Afrika na kuua watu takriban 100 katika nchi za Malawi na Msumbiji. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Kimbunga Freddy, kinachoelekea kuwa dhoruba ya muda mrefu iliyovunja rekodi ya kudumu, kilipiga sehemu za kusini mwa Afrika mwisho mwa wiki kwa mara ya pili ndani ya wiki chache, na kurejea tena baada ya mara kwanza kupiga katika eneo hilo mwishoni mwa mwezi.

Kimbunga hicho kililikumba eneo la kati la Msumbiji siku ya Jumamosi, na kuezua paa za majengo na kuleta mafuriko kuzunguka bandari ya Quelimane, kabla ya kuingia ndani kuelekea Malawi na mvua kubwa iliyosababisha maporomoko ya ardhi.

Kiwango kamili cha uharibifu na upotezaji wa maisha nchini Msumbiji bado hakijabainika, kwani umeme na simu zimekatika katika baadhi ya maeneo yalioathiriwa.

Dharuba hiyo imeua watu 99 nchini Malawi, wakiwemo 85 katika kituo kikuu cha kibiashara cha Blantyre, alisema kamishna wa Idara ya Masuala ya Kukabiliana na Maafa, Charles Kalemba, katika mkutano na waandishi wa habari.

Rais wa nchi hiyo Lazarus Chakwera alitangaza hali ya hatari katika eneo la Kusini mwa nchi hiyo baada ya kuelezea wasiwasi mkubwa kuhusu uharibifu uliosababishwa na kimbunga Freddy.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!