Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu
Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love

 

KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu atavaa viatu vyake vya uongozi pindi itakapotokea akafariki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tunduru … (endelea).

Amesema malengo ya chama hicho ni kushika dola hivyo kwa hatua waliyofikia na namna alivyomuandaa Ado ana uhakika kuwa atakiongoza chama hicho kuchukua madaraka.

Zitto ametoa kauli hiyo jana tarehe 13 Machi 2023 wakati akihutubia wananchi wa Tunduru mkoani Ruvuma katika mkutano wa hadhara.

Amesema; “Mimi ni kiongozi wa chama hiki, nina matamanio ya kuona nakipeleka chama kushika dola, lakini Mwenyezi Mungu naye ana mipango yake.

“Hata ikitokea leo Mwenyezi Mungu amesema bwana siku zako zimefika sasa nakuita, nitakwenda kwenye nyumba yangu ya milele nikiwa natabasamu,” amesema.

Amesema atakwenda akiwa anaamini kwamba ameacha mtu atakayeendeleza mapambano kama ambavyo Oliver Tambo alivyomuachia Nelson Mandela –(Afrika Kusini) au kama ambavyo Eduardo Mondlane alivyomuachia Samora Machel (Msumbiji) na huyo mtu ni Ado Shaibu.

Amewaomba wananchi hao kuwa ACT Wazalendo kiwe chama chao na sio suala la mjadala kufanya uamuzi tena.

Amesema chama hicho ndio chama kilichowathamini wana Tunduru kwa kumshika mkono mtoto wao (Ado) na kumpa majukumu mazito.

“Sasa nasema hata Mwenyezi Mumgu akinichukua sina wasiwasi… Ado atavaa viatu vyangu, ataendeleza mapambano mpaka tutakaposhika madaraka,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Ataka vifungu vinavyowabana vijana kugombea uongozi viondolewe

Spread the love  MWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo,...

error: Content is protected !!