Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema:Tutakuwa wajinga kukataa ruzuku kwa mazingira ya sasa
Habari za SiasaTangulizi

Chadema:Tutakuwa wajinga kukataa ruzuku kwa mazingira ya sasa

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, Rodrick Lutembeka
Spread the love

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kiko tayari kuchukua fedha za ruzuku kutoka Serikalini, kutokana na maridhiano yanayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akihojiwa na Kituo cha redio cha Wasafi FM, leo tarehe 19 Januari 2023, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Chadema, Rodrick Lutembeka, amesema watakuwa wajinga kama hawatapokeo kitu kinachotokana na maridhiano yanayofanyika kati ya Serikali na vyama vya siasa vya upinzani.

“Ikitokea kwa mazingira ya sasa hivi, sababu hata wakati ule wangeweza kuidumbukiza (akaunti ya benki) tusingeweza ichukua lakini kwa mazingira ya sasa hivi wakati tunaendelea na mazungumzo ya maridhiano Chadema tutakuwa wajinga sana kutoweza kupokea kile ambacho kinatokana na maridhiano.” alisema Lutembeka lipoulizwa kama Chadema kiko tayari kuchukua ruzuku.

Mkurugenzi huyo wa fedha Chadema, amesema malimbikizo ya fedha za ruzuku ambayo chama hicho kimegoma kupokea kutoka Serikalini tangu 2020, yamefikia zaidi ya Sh. 2 bilioni.

Amesema kuwa, Chadema kimekuwa kikijiendesha kupitia michango ya wanachama wake.

Akizungumzia kuhusu maridhiano yanayofanywa na Serikali pamoja na vyama vya siasa vya upinzani, Lutembeka ameeleza kuwa, matokeo yake yameanza kuonekana, ikiwemo kuondolewa zuio batili la mikutano ya hadhara, urekebishwaji wa sheria kandamizi ikiwemo sheria za uchaguzi, na ufufuaji mchakato wa upatikanaji katiba mpya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

error: Content is protected !!