Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa CUF: Hakutakuwa na ACT-Wazalendo Zanzibar uchaguzi 2025
Habari za Siasa

CUF: Hakutakuwa na ACT-Wazalendo Zanzibar uchaguzi 2025

Mhandisi Mohammed Ngulangwa, Mkurugenzi wa Habari -CUF
Spread the love

 

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeeleza kuwa kimejipanga kurejesha heshima yake visiwani Zanzibar, ifikapo 2025 kwa kuunda Serikali au kushiriki Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa jana tarehe 16 Januari 2023 na Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma CUF, Mhandisi Mohamed Ngulangwa, akizungumza na MwanaHALISI Online kwa simu, kuhusu kauli iliyotolewa na Chama cha ACT-Wazalendo, kwamba kimekufa.

“Nataka nikuhakikishie, hakutakuwa na ACT-Wazalendo kwenye Serikali ijayo, maana yake CUF kama hatukuchukua Serikali Zanzibar, tutakuwa tunaunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” amesema Mhandisi Ngulangwa.

Mkurugenzi wa Uenezi CUF, amesema kuwa chama chake kimeendelea kujiimarisha visiwani Zanzibar na Bara, na kwamba wanachama wake waliokimbilia ACT-Wazalendo kuanzia 2019, wameanza kurejea nyumbani.

“Mipango yetu tunaendelea nayo na tulikuwa tunaitumia mikutano ya hadhara, mwaka huu tunakamilisha uchaguzi wa ndani ya chama ikifika Oktoba tutapata safu ya uongozi itakayotusaidia kufanya vizuri katika chaguzi zijazo,” amesema Mhandishi Ngulangwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

error: Content is protected !!