Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa 25 wafariki dunia katika shambulizi Ukraine
Kimataifa

25 wafariki dunia katika shambulizi Ukraine

Spread the love

 

RAIS wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema idadi ya vifo kutokana na shambulio la kombora la Urusi kwenye jengo la ghorofa tisa katika mji wa kusini mashariki mwa Ukraine wa Dnipro imefikia 25. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Amesema hayo wakati waokoaji wakijaribu kuwaondoa manusura zaidi kutoka kwenye mabaki hayo.

Waokozi walitumia vifaa maalumu kujaribu kuwafikia watu waliokwama kwenye ghorofa za juu za jengo hilo lenye wakazi 1,700, ambao baadhi yao walitoa ishara ya kuomba msaada kwa taa za simu zao za mkononi.

Shughuli za utafutaji na uokoaji ziliendelea mpaka nyakati za mchana. Rais Zelenskyy aliahidi kupigania kila maisha ya watu waliokumbwa na shambulizi hilo.

Pia alisema watu 73 walijeruhiwa katika shambulio hilo juzi tarehe 14 Januari, 2023 huku 39 wakiokolewa jana alasiri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!