Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari ACT Wazalendo: CUF imekwisha
HabariHabari za SiasaTangulizi

ACT Wazalendo: CUF imekwisha

Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo
Spread the love

 

CHAMA cha ACT Wazalendo kimesema Chama cha Wananchi – CUF sio kwamba ushawishi wake kwa Watanzania umeshuka bali sasa umekwisha baada ya makada wake muhimu kuhamia ACT Wazalendo pamoja na majengo yao. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 16 Januari, 2023 na Katibu Mkuu wa ACT Waalendo, Ado Shaibu wakati akijibu swali kuhusu uhusiano ya chama hicho na vyama vingine vya upinzani.

Shaibu ambaye alikuwa akihojiwa katika Wasafi Redio, amesema uhusiani wa ACT Wazalendo na Chadema ni mzuri kwa sababu vyama hivyo vinategemeana katika kusukuma ajenda zao za kitaifa.

Akizungumzia uhusiano wa ACT Wazalendo na CUF, Shaibu amesema licha ya kwamba bado wana misuguano midogo ya hapa na pale, kwa uchambuzi wake anadhani CUF imekwisha.

“Tunadhani CUF imekwisha kwa sababu tukisema imeshuka ilihali pahala pao kule Zanzibar tumepachukua… hivyo ukifanya uchambuzi huru wa kisiasa ni Dhahiri kuwa maeneo yao tayari tumeyachukua.

“Kwangu kuzungumzia hali ya CUF wakati naona imekwisha si sahihi. Ninamheshimu Lipumba lakini ukizungumzia ukweli ndio huo,” amesema.

Shaibu amesema CUF wanafahamu Ofisi zao Zanzibar zilikuwa majengo ya watu ambao walitoa maghorofa na ofisi kubwa kubwa kutokana na imani yao kwa chama.

“Mtu yeyote atakayekwenda Zanzibar, ataona namna siasa za upinzani zilivyo juu. Ni watu wanaoenda msuli kwa msuli sawa na CCM na wakati mwingine kuzidi CCM.

“Sasa hawa wanachama wamehamia ACT Wazalendo, majumba yao yote wametuletea… kufumba na kufumbua mtu ulikuwa huna jengo Zanzibar, unaambiwa ofisi yako hii hapa, hilo ghorofa lote hapa Unguja ni la chama, ukienda Pemba maghorofa, kumbi za mikutano vivyo hivyo.

“CUF inasema hayo majengo ni yetu lakini wamiliki halali wanasema tuliwapa kwa sababu ya imani yetu CUF, imani imeondoka tumekwenda ACT Wazalendo na majengo tumekwenda nayo. Mahakamani wanaulizwa leteni hati… hawana, ni kesi nyepesi ambayo ilikuwa ni kupoteza muda tu,” amesema.

Kauli hiyo ya Ado imekuja siku chache baada ACT-Wazalendo kushinda kesi ya madai dhidi ya CUF katika Mahakama Kuu ya Zanzibar, Tunguu ambapo CUF walidai majengo yanayotumiwa na ACT-Wazalendo Zanzibar ni mali yao kabla ya wanachama wake, akiwemo aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kukihama chama hicho.

Kesi hiyo ilifunguliwa na CUF dhidi ya viongozi 20 wa ACT Wazalendo wakiongozwa na mdaiwa namba moja ambaye ni kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma CUF, Mhandisi Mohamed Ngulangwa, amekanusha madai hayo akisema chama chake hakiwezi kufa.

“Wao ndiyo wanasema, lakini hawawezi kutumaliza sababu sisi tunachukua kutoka kwao. Pemba wanachama wetu takribani asilimia 75 waliokwenda ACT-Wazalendo wamerudi kwetu na kazi inaendelea kila siku matawi yanafunguliwa,” amesema Mhandisi Ngulangwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaTangulizi

Mapya yaibuka wamasai waliohamishwa Ngorongoro kwenda Msomera

Spread the loveMAPYA yameibuka kuhusu zoezi la Serikali kuwahamisha kwa hiari wamasai...

Habari MchanganyikoTangulizi

Baba aomba msaada kuzika miili ya familia yake iliyofunga bila kula kuonana na Mungu

Spread the loveWAKATI Mamlaka nchini Kenya, ikiendelea kukabidhi miili ya watu waliofariki...

Habari za Siasa

Rais Samia ampongeza mpinzani aliyeshinda urais Senegal

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amempongeza mwanasiasa wa...

error: Content is protected !!