Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari Uhaba wa maji Musoma Vijijini kuwa historia kufikia Juni
Habari

Uhaba wa maji Musoma Vijijini kuwa historia kufikia Juni

Spread the love

 

HISTORIA ya uhaba wa maji kwa baadhi ya wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara, inatarajia kufutika ifikapo Juni 2023, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa bomba la maji la Mugango-Kiabakari-Butiama. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara…(endelea).

Hayo yamesemwa tarehe 14 Januari 2023 na Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi, wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, ilipokagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo, mkoani Mara.

“Tuko hapa kwenye mradi ambao unaenda vizuri na tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu na kujipongeza sisi watendaji wa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kazi tunayofanya ya kuwatua wanawake wa Mara ndoo kichwani. Serikali inawaletea maji kwa hiyo historia ya ukosefu wa maji itakwenda kupungua,” alisema Mahundi.

Kamati hiyo imeeleza kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo, ambapo Mjumbe wake, Almasi Maige, alisema “wito wangu kwa watu wa Mara kwanza tumsapoti Rais kwa maana ya kuthamini mradi wenyewe kusiwe na uharibifu wa miundombinu huko njiani ambako mradi unapita.”

Naye Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuongeza fedha kwa ajili ya kuhakikisha vijiji vyote vinavyonufaika na mradi huo kusambaziwa maji kwa awamu moja.

“Hivi juzi kwa kutekeleza agizo la Rais, vile vijiji ambavyo vingekuwa awamu ya pili vitapata maji kwa awamu moja kufuatia agizo la Rais kwamba hakuna awamu ya pili ni awamu moja na wamepewa fedha kiasi cha Sh. 4.7 bilioni. Kwa hiyo wakandarasi watajenga miundombinu kupeleka maji katika vijiji vyote,” alisema Prof. Muhongo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Mbunge Jimbo la Musoma Vijijini, mradi huo umegharimu Sh. 70 bilioni ambapo Serikali ya Saudi Arabia imetoa asilimia 49.12 ya fedha hizo huku Serikali ikitoa asilimia 19.48, wakati BADEA ikichangia asilimia 31.40.

Katika mradi huo, Serikali imetoa Sh. 4.7 bilioni kwa ajili ya kujenga miundombinu ya usambazaji maji kwenye Kata za Mugango na Tegeruka. Choteo la maji lililojengwa Kijiji cha Kwibara, Kata ya Mugango, Musoma Vijijini, lina uwezo wa kuchota lita 35 milioni kwa siku.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!