Monday , 6 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Masharti ya kudhibiti Covid-19 yapingwa kwa maandamano Urumqi
Kimataifa

Masharti ya kudhibiti Covid-19 yapingwa kwa maandamano Urumqi

Ma Xingrui
Spread the love

 

KATIBU wa Chama cha Kikomunisti cha Xinjiang, Ma Xingrui alifanya ziara katika mji mkuu Urumqi kaskazini-magharibi mwa China ambako maandamano ya kupinga hatua kuzuia watu wasitoke nje (lockdown) kutokana na maambukizi ya Uviko 19 kushamiri tena. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Maafisa wa polisi wa eneo hilo walithibitisha maandamano hayo kutokea ambapo waliwaadhibu wanaume watatu wa Kichina wa Han kwa kueneza uvumi juu ya changamoto ya upumuaji.

Ma Xingrui alitembelea wilaya na kaunti huko Urumqi iliyokumbwa na maambukizi mapya ya Uviko 19.

Ziara yake ilijumuisha wilaya za Tianshan, Shayibak, Shuimogou, High-tech Zone, na Midong za Urumqi, kufuatia maandamano ya wiki iliyopita ambapo ziara hiyo ililenga kukagua na kuchunguza hatua za kuzuia na kudhibiti janga, huduma za usimamizi wa jamii, na hospitali kwa mpango wa kuidhibiti Zinjiang kila siku.

Ma alisisitiza haja ya kutekeleza kwa uthabiti maamuzi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti na Baraza la Jimbo, na kuzingatia mkakati wa jumla wa kuzuia na kudhibiti janga.

Wakati huo huo, video mbili mpya za maandamano ya umma zilionekana kwenye mitandao ya kijamii mwishoni mwa wiki hii.

Katika video hizo, waandamanaji hao wanazungumza Kichina cha Mandarin, sio lugha inayozungumzwa na Wayghur wa asili wa Xinjiang, ambao wanakabiliwa na mateso kutoka kwa viongozi wa China katika eneo hilo.

“Usiogope! Uko sahihi! Leo lazima tuondoe kudhibitiwa (lockdown)!” waandamanaji wanasikika wakisema kwenye mojawapo ya video hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!