Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Biashara NMB, eGovernment Z’bar zakubaliana makubwa
Biashara

NMB, eGovernment Z’bar zakubaliana makubwa

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na Mkurugenzi Mtendaji wa Serikali Mtandao Zanzibar, Said Seif Said wakitiliana saini ya makubaliano ya ushirikiano wa ukusanyaji mapato na malipo ya Serikali kwa njia ya Kidigitali kwenye hafla iliyofanyika Zanzibar. Anayeshuhudia ni Mwanasheria wa Benki ya NMB, Lilian Komwihangiro (Kulia) na Mwanasheria wa Ofisi ya Serikali Mtandao Zanzibar, Safia Hija Abass (Kushoto).
Spread the love

BENKI ya NMB na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), kupitia Wakala wa Serikali Mtandao ‘eGovernment Zanzibar’ wamesaini makubaliano ya ushirikiano, yatakayowezesha mifumo ya benki hiyo kuingiliana na ile ya ZanMalipo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hatua hiyo itawezesha taasisi za SMZ kukusanya mapato kupitia matawi na mifumo ya kidijitali ya benki hiyo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na Mkurugenzi Mtendaji wa Serikali Mtandao Zanzibar,Said Seif Said wakionyesha mikataba baada ya kutiliana saini ya makubaliano ya ushirikiano wa ukusanyaji mapato na malipo ya Serikali kwa njia ya Kidigitali wakati wa hafla iliyofanyika Zanzibar. Kulia anyeshudia ni Mwanasheria wa Benki ya NMB, Lilian Komwihangiro na kushoto ni Mwanasheria wa Ofisi ya Serikali Mtandao Zanzibar, Safia Hija Abass

Hafla ya kusaini makubaliano hayo imefanyika Zanzibar leo Jumatano tarehe 16 Machi 2022.

NMB imesema imejipanga kuimarisha ushirikiano huo ambao utakuwa chachu ya ukuaji wa uchumi visiwani humo na inaamini utakuwa wa karibu zaidi, endelevu na wenye manufaa kwa SMZ na taasisi zake lakini pia utakaoleta maendeleo chanya.

Akizungumza kabla ya kusaini makubaliano hayo ya mwaka mmoja yenye kipengele kinachoruhusu mazungumzo na kuyarefusha, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, ameipongeza SMZ chini ya Rais Hussein Ali Mwinyi kwa mageuzi chanya ya kiuchumi yanayochakatwa na kusimamiwa na serikali yake kwa ustawi wa Taifa.

Ruth amesema makubaliano hayo ni chachu kwa taasisi yake kubuni suluhishi mbalimbali za Wazanzibar na Taifa ujumla na maendeleo ya kidijitali kwa ulimwengu wa sasa hayaepukiki, hivyo ushirikiano wao huo utakuwa na mchango chanya katika kuharakisha ukuzaji uchumi na kurahisisha utendaji wa Serikali.

“Makubaliano haya ni kielelezo tosha kuwa Serikali ya Zanzibar na NMB sasa tunaenda kushirikiana kuboresha huduma za ukusanyaji mapato na malipo, sambamba na kuwezesha mifumo yetu kuingiliana na ile ya ZanMalipo, hivyo kuwezesha Taasisi za SMZ kukusanya mapato kupitia matawi ya NMB na mifumo ya kidijitali ya benki yetu,” amesema Ruth.

 

“Kupitia makubaliano haya, NMB na eGovenment Zanzibar, tunaenda kutengenezea Kituo cha Pamoja cha Malipo Kidijitali ‘One Stop Center,’ cha Shirika la Bandari Zanzibar, ambacho kitampa mlipaji wa huduma mbalimbali ‘control number’ moja kwa ajili ya kufanyia malipo mbalimbili bandarini, badala ya namba tofauti tofauti.”

“Suluhisho hizi mbili zinazoambatana na makubaliano haya, zinaenda kuboresha utoaji huduma kwa wananchi, lakini pia kuongeza ufanisi katika ukusanyaji mapato na kuondoa kero ya muda mrefu wanaotumia wananchi kufanya huduma za malipo,” amesisitiza Ruth mbele ya wanahabari katika ukumbi wa Wizara ya Katiba na Sheria.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa eGovernment Zanzibar, Said Seif Said, ameishukuru NMB kwa kusaini makubaliano ya ushirikiano huo, ambao aliutaja kama muarobaini wa changamoto mbalimbali za kimalipo wanazokutana nazo wananchi wa Zanzibar, unaoenda pia kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali.

“Sisi eGovernment tunaamini ushirikiano huu ni chanya, utakaobeba tija kwa Serikali, hususani hiyo ‘One Stop Center’ ambayo itajikita katika kurahisisha mifumo ya malipo bandarini ambako tutatumia mifumo ya kidijitali kuongeza ufanisi kwenye makusanyo mbalimbali.

“Tunatarajia huu utakuwa ni mwanzo tu, tunategemea kufanya mengi makubwa kwa pamoja baina yetu na NMB. Bandarini ni sehemu ambako kumekuwa na changamoto za muda mrefu katika masuala mazima ya makusanyo, lakini kupitia makubaliano haya tunaamini yataondoa na kumaliza changamoto zote hizo,” amesema Seif.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

Biashara

Cheza kwa kuanzia Sh 400 kushinda mgao wa Expanse Tournament kasino 

Spread the love  UKISIKIA bosi kacheka ujue Maokoto yanafuatia, Kupitia promosheni pendwa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Biashara

Mchezo wa maokoto Cobra Queen unapatikana Meridianbet

Spread the love Meridianbet Kasino Mtandaoni utapata fursa ya kufurahiamchezo uliochochewa na...

error: Content is protected !!