Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Kitaifa Dk. Ndumbaro awavisha vyeo viongozi TANAPA, NCAA
KitaifaUtalii

Dk. Ndumbaro awavisha vyeo viongozi TANAPA, NCAA

Spread the love

Dk. Ndumbaro awavisha vyeo viongozi TANAPA, NCAA

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Damas Ndumbaro leo tarehe 18 Februari, 2022 ameongoza zoezi la uvishaji vyeo kwa Viongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA). Anaripoti Gabriel Mushi … (endelea)

Viongozi waliovishwa vyeo hivyo ni William Mwakilema ambaye hivi karibuni aliteiliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Viongozi wengine waliovishwa vyeo ni kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) ambao ni Needpeace Wambuya aliyepandishwa cheo kuwa Naibu kamishna wa Uhifadhi (Huduma za Shirika) na Elibariki Bajuta aliyepandishwa cheo kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi (Huduma za Ulinzi).

Akizungumza baada ya Dk. Ndumbaro kuwavalisha vyeo hivyo Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Francis Michael ameagiza viongozi wote wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kuhakikisha watumishi wote wa taasisi hizo wanakwenda kupata mafunzo ya kijeshi kwa muda wa miezi mitatu ili kukidhi matakwa ya sekta ya utalii kuwa jeshi la hifadhi.

Pia ameagiza viongozi wa taasisi hizo kuhakikisha watumishi wote wanavaa sare za kijeshi kulingana na wadhifa wao.

Licha ya kuipoingeza TANAPA kwa mafanikio makubwa iliyoyafikia katika kuboresha sekta ya utalii nchini, pia amehimiza watumishi wa sekta hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariKitaifa

Mabasi ya New Force yapigwa kitanzi kisa ajali

Spread the loveMAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imefuta ratiba za safari...

HabariKitaifa

Spika Tulia aeleza sababu za kengele ya hatari kulia Bungeni

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amesema kengele ya hatari...

HabariKitaifaTangulizi

Ni Bajeti ya kulipa madeni, mzigo wa kodi

Spread the love WAZIRI wa fedha, Mwigulu Nchemba, amewasilisha bajeti ya serikali...

Kitaifa

Serikali yatenga eka 10 kwa kila kijana mwenye sifa kufanya kilimo

Spread the love  SERIKALI nchini Tanzania imetenga eka 10 kwa kila kijana...

error: Content is protected !!