Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Kitaifa Serikali yatenga eka 10 kwa kila kijana mwenye sifa kufanya kilimo
Kitaifa

Serikali yatenga eka 10 kwa kila kijana mwenye sifa kufanya kilimo

Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania
Spread the love

 

SERIKALI nchini Tanzania imetenga eka 10 kwa kila kijana atakayechaguliwa kujiunga na mafunzo ya kilimo na baadae kushiriki katika kilimo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hayo yameelezwa na Rais Samia Suluhu Hssan wakati akijibu swali kuhusu namna ya kuvutia vijana kwenye kilimo, upatikanaji wa ardhi, teknolojia na fedha wakati wa ufunguzi wa mkutano unaohusu kilimo unaofanyika Dakar nchini Senegali.

Rais Samia amesema Tanzania ipo katika mchakato wakupokea maombi ya kwa kundi la kwanza la vijana watakaopata fursa ya kupata mafunzo ya miezi mitatu kuanzaia katikati ya mwezi Februari na kisha wagaiwe ardhi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhurua Yunus jana, Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) imetangaza kutoa mkopo wad ola za Marekani 120 milioni kwa ajali ya sekta ya kilimo ikiwemo umwagiliaji na kujenga kituo cha usafirishaji na usambazaji mbolea.

Taarifa hiyo imesema mpango huo unalenga vijana na wanawake ujulikanao kwa jina BBT “ujenzi wa kesho bora” umeanzisha mfuko wa dhamana kwa vijana na huduma za mikopo nafuu chini ya mfuko wa Pembejeo.

Rais Samia amesema Tanzania iemamua kuanzisha mpango huo kutokana na idadi kubwa ya vijana kukosa sifa zinazohitajika na taasisi za fedha wanapoomba mikopo.

“Tangu kuanzishwa kwa mpango huo wa BBT miezi sita iliyopita, tayari imeweza kutenga eka 600,000 kwa nchi nzima na shughuli ya kusafisha mashamba hayo imeanza,” imeeleza taarifa ya Yunus

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariKitaifa

Mabasi ya New Force yapigwa kitanzi kisa ajali

Spread the loveMAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imefuta ratiba za safari...

HabariKitaifa

Spika Tulia aeleza sababu za kengele ya hatari kulia Bungeni

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amesema kengele ya hatari...

HabariKitaifaTangulizi

Ni Bajeti ya kulipa madeni, mzigo wa kodi

Spread the love WAZIRI wa fedha, Mwigulu Nchemba, amewasilisha bajeti ya serikali...

Habari MchanganyikoKitaifa

Wananchi KIA walia kunyang’anywa ardhi

Spread the loveWANANCHI wa vijiji vinavyozunguka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa...

error: Content is protected !!