Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari Spika Tulia aeleza sababu za kengele ya hatari kulia Bungeni
HabariKitaifa

Spika Tulia aeleza sababu za kengele ya hatari kulia Bungeni

Spika Dk. Tulia Ackson
Spread the love

SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amesema kengele ya hatari iliyofanya mhimili huo usitishe shughuli zake kwa muda, imetokana na marekebisho yaliyokuwa yanafanywa katika sehemu ya chimi ya ukumbi wake, yaliyosababisha vumbi na kupelekea mifumo ya usalama kuhisi kuna moshi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Spika Tulia ametoa taarifa hiyo leo Jumanne, muda mfupi baada ya kikao cha Bunge kurejea.

“Hitilafu imetokana na kwamba walikuwa wanafanya marekebisho ilidi watindue eneo, katika kutindua vumbi ikatoka na vinavyonasa hitilafu ikanasa ile vumbi kama moshi. Kwa hiyo ndiyo maana ikapiga kelele kuashiria kuna shida kwenye jengo hili,” amesema Spika Tulia.

Spika Tulia amewatoa hofu wabunge na wananchi kwamba changamoto hiyo imedhibitiwa na kwamba marekebisho yanaendelea kwa utaratibu mzuri.

Kengele ya dharura ililia wakati Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, anajibu maswali ya wabunge. Ambapo Spika Tulia aliahirisha kikao hicho kwa muda na kuwataka wbaunge watoke nje ya ukumbi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!