Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Kikao cha Bunge chaahirishwa ghafla, larejea
GazetiHabari

Kikao cha Bunge chaahirishwa ghafla, larejea

Spread the love

KIKAO cha Bunge kilichokuwa kinaendelea leo Jumanne, tarehe 27 Juni 2023, kimeahirishwa ghafla baada ya kutokea dharura. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Kikao hicho cha 56 cha mkutano wa 11 wa Bunge la 12, kimeahirishwa na Spika Dk. Tulia Ackson, baada ya kengele ya dharura kulia wakati Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, anajibu maswali ya wabunge.

Baada ya kengele hiyo kulia, Spika Tulia alimkatisha Mhandisi Kasekenya, na kuwaelekeza wabunge watoke nje ya ukumbi wa bunge hadi dharura hiyo itakapopatiwa ufumbuzi.

“Naibu waziri na wabunge nadhani hiyo inaashiria tutoke humu ndani kwa haraka, kila mtu afuate mlango ulio karibu yake haraka tutoke. Sote twende sehemu ile ya kukusanyika watu, naahirisha mpaka jambo hili litakaporekebishwa,” amesema Spika Tulia.

Hata hivyo, baada ya muda mfupi Bunge lilirejea, ambapo Spika Tulia amesema atatoa taarifa kuhusu tukio hilo baadae.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!