Saturday , 4 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kikao cha Bunge chaahirishwa ghafla
Habari za SiasaTangulizi

Kikao cha Bunge chaahirishwa ghafla

Spread the love

KIKAO cha Bunge kilichokuwa kinaendelea leo Jumanne, tarehe 27 Juni 2023, kimeahirishwa ghafla baada ya kutokea dharura. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Kikao hicho cha 56 cha mkutano wa 11 wa Bunge la 12, kimeahirishwa na Spika Dk. Tulia Ackson, baada ya kengele ya dharura kulia wakati Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, anajibu maswali ya wabunge.

Spika Dk. Tulia Ackson

Baada ya kengele hiyo kulia, Spika Tulia alimkatisha Mhandisi Kasekenya, na kuwaelekeza wabunge watoke nje ya ukumbi wa bunge hadi dharura hiyo itakapopatiwa ufumbuzi.

“Naibu waziri na wabunge nadhani hiyo inaashiria tutoke humu ndani kwa haraka, kila mtu afuate mlango ulio karibu yake haraka tutoke. Sote twende sehemu ile ya kukusanyika watu, naahirisha mpaka jambo hili litakaporekebishwa,” amesema Spika Tulia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!