Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Biden asisitiza kuwa Rais Xi Jinping ni ‘Dikteta’
Kimataifa

Biden asisitiza kuwa Rais Xi Jinping ni ‘Dikteta’

Xi Jinping, Rais wa China
Spread the love

 

RAIS wa Marekani Joe Biden amesisitiza kuwa ataendelea kumwita Rais wa China Xi Jinping ‘Dikteta.’  Imeripotiwa na VOA … (endelea).

Biden alitoa kauli hiyo Ijuma lililopita alipoulizwa kuhusu taarifa hiyo wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na Waziri Mkuu Narendra Modi na kueleza kuwa hatabadilisha kauli hiyo.

Biden alisema anaamini kuwa uhusiano kati ya China na Marekani hauko sawa tofauti na uhusiano wake na India.

Sisi na India kuna heshima kuwa sehemu moja kwa sababu sisi sote tunaheshumu Demokrasia “, alinukuliwa Biden.

Wanadiplomasia duniani wanaeleza kuwa sio jambo la kushangaza tena kwa Rais Biden kuzungumza waziwazi kuhusu tofauti ya nchi yake na China.

Akihutubia mkutano wa kuchangisha pesa za kampeni huko California, Biden alizungumza juu ya puto ya China iliyoingia kwenye anga ya Amerika, na kudhoofisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili kwa miezi.

Alisema mashirika ya kijasusi ya Marekani yamejifunza kuhusu mkanganyiko wa ndani huko Beijing wakati wa tukio hilo.

Biden alisema, “Hiyo ni aibu kubwa kwa madikteta wakati hawakujua kilichotokea,” Akijibu kauli ya Rais wa Marekani, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning, alimshutumu Joe Biden kwa “uchochezi wa kisiasa.”

Joe Biden

Akijibu swali kuhusu matamshi yaliyotolewa na Biden hivi majuzi, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China alisisitiza msimamo wa serikali yake kwamba tukio la puto lilikuwa tukio la bahati mbaya.

Akihutubia kikao cha wanahabari siku ya Jumatano, msemaji wa Mambo ya Nje wa China Mao alisema matamshi yaliyotolewa na Rais wa Marekani ni ya kipuuzi , hayana ukweli wowote na yamekwenda kinyume cha misingi ya kidiplomasia na heshima ya kisiasa nchini China.

“China hairidhishwi na inapinga vikali jambo hili.” Alisema Mao.

Kauli ya Biden imekuja siku chache baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kutembelea China. Ingawa ziara ya Blinken ya Beijing haikuleta mafanikio makubwa zaidi ya makubaliano yake na y Xi ya kuleta utulivu kati ya China na Marekani.

Ziara ya Blinken huko Beijing ilipangwa hapo awali Februari ambapo iliahirishwa baada ya puto ya China kuvuka kwenye anga ya Amerika.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imekanusha dhana kwamba matamshi ya Biden hayakuwa na tija kwa juhudi za Blinken.

Akihutubia mkutano na wanahabari Jumatano, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Vedant Patel alisema, kuwa Marekani itaendelea mawasiliano na Serikali ya China.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!