Akizungumza bungeni mjini Dodoma leo Alhamisi, tarehe 15 Juni, Mwigulu alisema,katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/24, serikali imepanga kutumia jumla ya Sh. 44.39 trilioni.
Kati ya fedha hizo, Sh. 6.31, zitatumika kulipia deni la taifa, huku Sh. 11.89 trilioni zikipelekwa kutoa huduma za utawala.
Katika sekta ya elimu kwa ujumla wake, serikali imepanga kutumia kiasi cha Sh. 5.95, ulinzi na usalama, Sh. 4.68 trilioni; ujenzi, usafirishaji na mawasiliano, Sh. 3.84 trilioni na nishati ikipangiwa kutumika Sh. 3.05 trilioni.
Kwa upande wa hifadhi ya jamii, serikali imetenga kiasi cha Sh. 2.35 trilioni, kilimo Sh. 1.47 trilioni, nyumba na maendeleo ya jamii, Sh. 1.34 trilioni na shughuli nyingine za maendeleo ya uchumi kumetengwa kiasi cha Sh. 1.07 trilioni.
Aidha, Mwigulu aliomba Bunge la Jamhuri, kupitisha kodi mpya ya Sh.100 kwa kila lita ya mafuta ya dizeli na petroli itakayouzwa nchini, hatua ambayo inakosolewa na baadhi ya wananchi.
“Kupata kodi ni lazima uwekeze, lakini serikali yetu haina akili hiyo ya kufanya uwekezaji mkubwa. Ndio maana kila mwaka, wanakimbilia sekta kama mafuta au pombe, maana kule ni rahisi kukusanya bila kuwekeza chochote,” anaeleza Fabian Joshua, mfanyabiashara na mkazi wa Mkuyuni, mjini Dodoma.
Anasema, “wangewekeza kwenye utalii. Kule kuna billioni za kutosha bajeti nzima ya nchi ingetoka huko. Lakini maarifa yao ndio yameishia hapo tuu na hawataki kazi ngumu.”
Naye Fatuma Juma, mkazi wa Kinodoni, Dar es Salaam, ameshutushwa na hatua ya serikali ya kuweka kodi hiyo kwenye mafuta.
Anasema,”siungi kodi hii, kwa kuwa ripoti ya Mkagugi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeonyesha kuna wizi mkuwa wa fedha za umma, ambazo ni kodi za wananchi.”
Anaongeza, “badala ya wananchi kuongezewa kodi hii, wakati bado wana mizigo mikubwa, serikali ingejikita katika kushughulikia wizi unaofanyika.”
Hii ni bajeti ya pili, tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, Machi mwaka juzi. Rais Samia aliapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 19 Machi 2021. Alichukua wadhifa huo kufuatia kifo cha mtangulizi wake, John Pombe Magufuli.
Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, Rais Samia atahudumu hadi Oktoba 2025, pale uchaguzi mwingine wa urais utakapofanyika.
Spread the love JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...
By Mwandishi WetuApril 27, 2024Spread the love RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...
By Masalu ErastoApril 27, 2024Spread the love MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...
By Mwandishi WetuApril 26, 2024Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...
By Mwandishi WetuApril 26, 2024
Leave a comment