Monday , 6 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya  NMB yaunga mkono uchangiaji damu salama Morogoro, Dodoma
Afya

 NMB yaunga mkono uchangiaji damu salama Morogoro, Dodoma

Spread the love

BENKI ya NMB imeadhimisha wiki ya uchangiaji damu salama kwa hiari baada ya kuwakusanya watumishi wa benki hiyo pamoja na wananchi katika mikoa ya Morogoro na Dodoma kwa lengo la kuungana mkono jitihada za Wizara ya afya za kupunguza changamoto ya upatikanaji wa damu salama. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Jitihda za benki hiyo zinalenga kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa kupungukiwa na damu hapa nchini.


Akizungumza katika hasama ya uchangiaji damu salama kwa hiari mjini hapa, Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Tanzania mkoa wa Morogoro, Ileme Wilson aliesema uhitaji wa damu salama katika hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro ni kati ya uniti 350 hadi 400 kwa mwezi ili kuokoa maisha ya watoto wachanga, akinamama wanaojifungua na wahanga waliokumbwa na ajali za aina mbalimbali.

Wilson alisema hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro hutumia uniti 15 kwa siku za damu salama ili kukabiliana na wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu hasa kundi la watoto wachanga, akinamama wanaojifungua na wahangana waliopata ajali na wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji.

“Niwapongeze benki ya NMB Morogoro kwa maamuzi ya kuwakusanya watumishi wao pamoja na wananchi kuwahamasisha kuchangia damu salama maana yake wanaungana na mpango wa wizara ya afya ya kuwaomba wananchi kuchangia damu salama kwa ajili ya kunusuru vifo vinavyotokana na upungufu wa damu kwa wagonjwa katika hospitali zetu hapa nchini,” aliesema Wilson.

Wison alisema hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro kwa sasa ina akiba ya uniti 200 za damu ikiwa ni pungufu ya uniti 200 zinahitajika kila mwezi ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu.

Mmoja wa watumishi wa benki hiyo, Afsa Abeid alisema mpango ulioanzishwa na wakubwa zao ni nzuri kwani unalenga kuokoa maisha ya wagonjwa ambao wana uhitaji wa damu pale wanapoumwa na kulazwa.

“Mpango huu wa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wenzetu ambao wana uhitaji mi muhimu. Natumia fursa hii kuupongeza uongozi wetu wa NMB kwa kutuhamasisha sisi watumishi kuchangia damu salama,” aliesema Afsa.

Meneja wa Benki ya NMB tawi la Mount Uluguru, Lilian Abraham alisema benki hiyo imeungana na wizara ya afya katika maadhimisho ya siku za uchangiaji damu kwa hiyari kitaifa inayoanza kuadhimishwa kuanzia Juni Mosi hadi Juni 14 kwa kushirikiana na mpango wa taifa wa damu salama Tanzania Morogoro.

Katika hatua nyingine, Benki ya NMB jana ilifungua pazia la wiki ya kuchangia damu kwa kuwaongoza kundi la watu kuchangia damu katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Afisa Mwajili wa Kanda ya Kati Braison Tarimo aliongoza jopo la wafanyakazi,wadau,wafanyabiashara na wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma katika zoezi lilitajwa kuwa na mafanikio makubwa.

Tarimo alisema NMB waliamua kwa hiyari yao kuungana na Watanzania katika kusaka njia ya kuokoa maisha ya watu hasa wanawake ambao hupoteza maisha wanapojifungua kwa kukosa damu.

Alisema uamuzi wa benki hiyo sasa utakuwa ni endelevu na watakuwa wakiwahamasisha wadau na wateja wao kuona umuhimu wa kujitolea kuchangia damu kila inapobidi badala ya kusubiri kuwepo kwa matatizo ya kiuhitaji.

“Tumekuja kuchangia damu leo, hii itakuwa ni moja ya mipango yetu kuanzia sasa na utakuwa ni mpango endelevu, lazima tusaidie kuokoa maisha ya wenzetu hasa wakina mama na watu wanaokutana na ajali,’ alisema Tarimo.

Meneja wa NMB Tawi la Dodoma Amos Mgusi yeye alisema mwitikio mkubwa walioonyesha wateja wao na watumishi wa benki ni kielelezo tosha kuwa jambo hilo ni la muhimu sana katika maisha ya watu.

Mgusi alisema walikuwa wamewaalika wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Chuo cha Mipango, Chuo Kikuu cha St John’s na Chuo cha Bishara (CBE) Tawil la Dodoma na wote walishiriki kwa wingi lakini wakaungwa mkono na wafanyabiashara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

error: Content is protected !!