Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT Wazalendo watahadharisha mkataba wa EPA, watoa mapendekezo 5
Habari za Siasa

ACT Wazalendo watahadharisha mkataba wa EPA, watoa mapendekezo 5

Bendera ya ACT-Wazalendo
Spread the love

 

CHAMA cha ACT Wazalendo kimependekeza kuwa kabla ya kusainiwa mkataba wa EPA, serikali ihakikishe kuna mfumo wa kufidia upotevu wa mapato yatokanayo na kupunguzwa au kuondoshwa kwa ushuru wa uingizaji na utoaji wa bidhaa kwani kwa makubaliano ya sasa Umoja wa nchi za Ulaya ulikataa kulipa fidia za upotevu huo wa mapato. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

EPA – (European Partnership Agreement) ni makubaliano ya kiuchumi yanayolenga kuunda eneo huru la biashara kati ya nchi za umoja wa Ulaya (EU) na mataifa ya Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Kisekta -Wizara ya Viwanda na Maendeleo ya Biashara, Halima Nabalang’anya pia imesema mkataba usainiwe na Afrika (AU) nzima kwa umoja wetu.

Ameshauri kuwa mkataba huo usainiwe na nchi za Afrika chini ya Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Ulaya kupitia Soko Huru la Afrika (AfcFTA) ambayo sasa Tanzania ni mwanachama wake.

“Hii itawezesha kuwa na eneo pana la uhuru wa biashara ndani ya Afrika na Tanzania kuwa na mahusiano na nchi hizo. Pia, kupitia njia hiyo Afrika itakuwa na sauti zaidi kuliko ilivyo sasa ambapo Afrika imegawanywa gawanywa katika kambi 7 kupitia jumuiya za kikanda ili kujiunga na EPA,” amesema.

Pendekeza la tatu ni kwamba Serikali ije na mkakati unaoeleweka wa kufidia mapato ya moja kwa moja yatakayopotea kutokana na kuingia makubaliano ya EPA.

“Mkataba huu kwa kiasi kikubwa utafunga au kuminya uhuru wa biashara kati ya nchi yetu na nchi nyingine kwa baadhi ya bidhaa ili kutoa kipaumbele kwa EPA na kufanya nchi yetu isiweze kuagiza bidhaa kutoka katika nchi hizo jambo ambalo ni wazi litaikosesha Serikali mapato” amesema.

Pia kanuni ya ‘Variable Geometry’ itumike kupunguza athari hasi za mkataba huo.

“Tunashauri Serikali ifanye majadiliano na Umoja wa Ulaya (EU) ili nchi yetu au nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ziwe na fursa ya kutumia kanuni ya “Variable Geometry” yaani kuwa na uhuru wa kuchagua vifungu vya kutekeleza na kuacha vile ambavyo vinaonekana kuhatarisha maslahi ya nchi kibiashara na kiuchumi hadi pindi vitakapofanyiwa maboresho au marekebisho.

“EU haipaswi kulazimisha nchi zote za Jumuiya kuridhia kwa pamoja kwani kila Taifa lina maslahi yake tofauti,” amesema.

Pendekezo la mwisho ni kwamba fursa ya Ukanda wa Soko Huru la Afrika (AfcFTA) haijatumika ipasavyo.

“Tunaishauri Serikali kuelekeza juhudi zaidi katika kuchangamkia fursa ya nchi yetu kunufaika zaidi na fursa ya AfcFTA ambayo Tanzania ni mwanachama wake.

“Pamoja na masoko yanayopatikana kupitia Jumuiya zetu za kikanda EAC na SADC, bado tumeonesha kulegalega katika kuitumia fursa hiyo.

“Ni maoni yetu kuwa, tunaweza kushindana ipasavyo na nchi ambazo angalau tuna mlingano wa kiuchumi (at least equal level of economy) kuliko nchi za Jumuiya ya Umoja wa Ulaya ambazo zimetuzidi kwa viwango vikubwa,” amesema.

Mapendekezo hayo ya ACT Wazalendo yamekuja siku chache baada ya Rais wa Samia Suluhu Hassan kukutana na Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Charles Michel mara baada ya kuwasili tarehe 15 Februari, 2022, katika Makao Makuu ya Baraza hilo mjini Brussels, Ubelgiji na kueleza utayari wa Tanzania kufanya mkutano wa maridhiano hayo.

Katika taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, ilisema mwanzoni mwa mwezi Machi 2022 Tanzania itafanya mkutano wa maridhiano na kupitia upya makubaliano ya mkataba wa EPA kati ya nchi za Afrika Mashariki na Umoja wa nchi za Ulaya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!