Tuesday , 30 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri ataja chanzo mabucha ya nyamapori kusuasua
Habari Mchanganyiko

Waziri ataja chanzo mabucha ya nyamapori kusuasua

Spread the love

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro amesema chanzo cha maduka ya nyamapori kuzorota nchini, ni wafanyabiashara waliopewa leseni za biashara hiyo kushindwa kutafuta nyama za kutosha kutoa huduma kwa wananchi.

Pia amesema licha ya kutoa leseni nyingi kwa wafanyabiashara hao, tatizo hawakumuelewa lakini wizara inaendelea kutoa elimu kuhusu namna ya kutoa huduma hiyo kwa njia sahihi. Anaripoti Gabriel Mushi … (endelea).

Waziri huyo ametoa kauyli hiyo leo tarehe 18 Februari, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu mafanikio na changamoto za wizara hiyo.

“Sisi tulitoa leseni kwa wafanyabiashara ili wapate uhalali wa kuuza nyama hizo, lakini suala la upatikanaji wa nyama ni jukumu lao, wanaweza kupata nyama hizo kwa kufuga kwenye mashamba yao kwa vibali maalumu au kwa kununua kwa wenye vitalu vya uwindaji.

“Sasa cha ajabu walitegemea sisi Serikali tuwape leseni ya kuuza nyama na nyama tuende kuwatafutia tuwapatie! Kwa hiyo bado tunaendelea kuwapa elimu kwa sababu leseni za maduka zimegawiwa kwa wingi lakini wafanyabiashara hao hawana nyama,”
amesema.

Akizungumzia kuhusu hatima ya Serikali kuhusu Cable Car kwa ajili ya kupanda Mlima Kilimanjaro, Dk. Ndumbaro amesema mwezi ujao kuna mkutano maalumu kwa ajili ya kujadili suala hilo na kulipatia muafaka.

Amesema suala hilo linahitaji mjadala mpana ili kufikia muafaka.

Tarehe 21 Disemba, 2020 bucha la kwanza la kuuza nyamapori lilifunguliwa mkoani Dodoma kufuatia agizo la Rais wa awamu ya tano, Dk. John Magufuli alilolitoa mapema mwaka huo la kuwa na mabucha ya nyama hizo.

Akizungumza wakati wa kufungua bucha hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko alisema bucha hilo limekuwa la kwanza kati ya 46 yaliyopata  usajili.

Mabucha hayo yalipata usajili baada ya Kamati ya Kumshauri Kamishna kuhusu bucha za kuuza nyamapori kuridhia kufuatia kanuni ya bucha ya mwaka 2020 ambayo iliundwa baada ya tamko la Rais Magufuli la mwezi Machi mwaka huu kutaka kuanzishwa bucha za nyamapori Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TMA yapongezwa kuimarisha ubora na usahihi wa taarifa za Hali ya Hewa

Spread the love  WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

7 wafa Ulanga, mbunge alia kutelekezwa na mawaziri, Tanroad

Spread the loveWatoto saba wamepoteza maisha na zaidi ya kaya 70 kukosa...

Habari Mchanganyiko

Bil 12.4 zimetumika ujenzi wa miradi wilaya ya Momba

Spread the love MKUU wa wilaya ya Momba mkoani Songwe Kennan Kihongosi...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

error: Content is protected !!