Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko ‘Royal tour’ yapaisha mapato ya utalii 2021
Habari MchanganyikoUtalii

‘Royal tour’ yapaisha mapato ya utalii 2021

Spread the love

WAKATI filamu ya kihistoria ya “THE ROYAL TOUR” ambayo Rais Samia Suluhu Hassan ameshiriki akiwa Mwongozaji Mkuu wa watalii ikitarajiwa kuzinduliwa rasmi Aprili mwaka huu, matunda ya maandalizi ya filamu hiyo yamejitokeza baada ya mapato ya sekta ya utalii nchini kupanda kutoka Dola za Marekani milioni 714.59 mwaka 2020 hadi kufikia dola bilioni 1.2544 mwaka 2021.

Pia matunda ya filamu hiyo ambayo Rais Samia alishiriki kwa lengo la kutangaza utalii, uwekezaji na nyanja nyingine zikiwemo urithi wa sanaa na utamaduni wa Taifa, imevutia idadi ya watalii wa nje  kutoka 620,000 mwaka 2020 hadi kufikia watalii wa nje 922,692. Anaripoti Gabriel Mushi… (endelea)

Hayo yamebainishwa leo tarehe 18 Februari, 2022 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu mafanikio na changamoto za wizara hiyo.

Amesema mafanikio hayo yamefikiwa licha ya mwaka 2020/2021 kuwa mwaka ambao sekta ya utalii imeathiriwa pa kubwa na janga la maambukizi ya ugonjwa wa Covid -19 na kusababisha sekta ya utalii duniani kuporomoka kwa asilimia 72.

Amesema wakati hayo yakitokea duniani, idadi ya watalii wa ndani kwa upande wa Tanzania imeongezeka na kufikia 788,933 idadi ambayo haijawahi kufikiwa tangu Tanzania ipate uhuru wake mwaka 1961.

Aidha, ameongeza kuwa asilimia 70 ya watalii hao wa ndani ni wanawake hivyo hiyo ni changamoto kwa wanaume nao kuchangamkia fursa kwa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Amesema licha ya janga hilo la Corona, kiujumla sekta ya utalii imechangia asilimia 17.6 ya pato la Taifa mwaka 2021 wakati sekta ya misitu ikichangia asilimia 3.5 na kuifanya wizara hiyo kiujumla kuchangia asilimia 21 ya pato la Taifa.

Pia sekta hiyo ya maliasili na utalii ambayo imechangia ajira milioni 6.6, pia imchangia asilimia 25 ya fedha za kigeni.

Ameongeza kuwa kutokana na mafanikio hayo, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya utalii (UNWTO) limeitangaza Tanzania kuwa nchi iliyopiga hatua na kuwa namba moja duniani katika sekta ya utalii kwenye kipindi hiki cha janga la Corona.

Amesema kutokana na mafaniklio, Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa Shirika hilo unaotarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu.

MAKAMPUNI 30 YABISHA HODI

Amesema muda mfupi baada ya filamu hiyo ya Royal tour kuanza kurekodiwa, jumla ya makampuni 30 kutoka Marekani na Barani Ulaya yamejitokeza kuja kuleta watalii nchini.

Pia ameongeza kuwa kampuni moja kutoka nchini Bulgaria nayo imejitokeza kuwekeza katika ujenzi wa hoteli za nyota tano sawa na Kilimanjaro Kempisk katika mbuga za Tarangire, Serengeti, Manyara na Ngorongoro.

Pamoja na mambo mengine amesema sekta hiyo ya utalii imefaniwa kupata tuzo 10, tuzo za za heshima nne.

Amesema malengo ya wizara hiyo na Taifa kwa ujumla ni kuwa nchi ya kwanza duniani kwa kuwa na watalii wengi kama ilivyo nchi ya Hispania ambayo hata hivyo haina vivutio vya kipekee kama ilivyo Tanzanzania.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!