Monday , 6 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu GGML yamwaga milioni 248 kuwezesha watumishi wake kuhitimu Shahada ya uzamili
ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yamwaga milioni 248 kuwezesha watumishi wake kuhitimu Shahada ya uzamili

Spread the love

 

JUMLA ya watumishi waandamizi 18 wa kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) wamehitimu Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara kutoka Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) kwa gharama ya zaidi ya Sh milioni 248. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Hayo yameelezwa na juzi na Makamu wa Rais wa GGML, Simon Shayo wakati akizungumza katika mahafali hayo yaliyofanyika katika viwanja vya ESAMI jijini Arusha ambapo watumishi tisa waandamizi wa Kampuni hiyo walihitimu.

Watumishi hao tisa wanafanya idadi ya watumishi waliofadhiliwa na kampuni hiyo ya GGML kuwa 18 tangu mpango huo wa masomo ulipoanza mwaka 2018.

Alisema hatua hiyo imeiwezesha GGML kuwa na watumishi kadhaa wa Kitanzania walioteuliwa kushika nyadhifa za juu.

Alisema hatua hiyo inaenda sawa na malengo ya kuifanya kampuni kuwa na watumishi wa Kitanzania wanaosimamia idara mbalimbali ndani ya kampuni na kutekeleza majukumu yako kwa uweledi na ufanisi mzuri.

“Kampuni imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kubaini vipaji vya watumishi wake watanzania hususani kupitia mpango stashahada ya uzamili (Postgraduate diploma) kutoka Shule ya Biashara ya Regenesys ya Afrika Kusini.

“Zaidi ya wafanyakazi 50 wa ngazi ya juu na wa kati wamefadhiliwa na kuhitimu programu hiyo tangu 2016,” alisema.

Alisema katika jitihada za kuwawezesha wanawake nao kushika nyadhifa za juu, GGML imebuni programu zinazowawezesha wanawake kupiga hatua.

“Kwa muda wa miaka minne iliyopita, idadi ya wafanyakazi wetu wanawake wameshiriki katika Mpango wa ‘Mwanamke Baadaye’ unaotekelezwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ambapo wanne walioshiriki katika mpango huu wamehitimu mwaka huu.

“Kampuni pia inashiriki katika program ya kuwaandaa vijana kuwa viongozi ambao unashirikisha vijana wa kike na wa kiume,” alisema.

Aidha, mmoja wa wahitimu tisa katika mahafali hayo, Mhandisi Mkuu kutoka GGML, Seif Maftah ambaye alihitimu Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara alisema ufadhili huo wa GGML umekuja wakati mwafaka.

“Nimefurahi na ninahisi kuwa na bahati ya kipekee kupata fursa hii. Kampuni yetu imekuwa mstari wa mbele kuwaongezea uwezo watumishi wake mbali na faida na ushindani kwa rasilimali zake za ndani. Kozi hii imeniwezesha kuongeza ujuzi wangu, hasa usimamizi wa fedha,” alisema Mhandisi Maftah.

Naye Ofisa Rasilimali watu kutoka GGML, Hamza Ngunangwa ambaye pia amehitimu alisema, “Nimefurahi  kuhitimu licha ya changamoto za COVID-19, nawapongeza ESAMI kwa kuanzisha madarasa ya mtandaoni. Hii ilitusaidia.

“Pia uongozi wa GGML ulitupatia likizo ya masomo ambayo ilituwezesha kukamilisha kozi hii. Lakini pia niwapongeze wahitimu wenzangu kwa kutiana moyo katika kipindi chote cha masomo yetu,” alisema

Kwa upande wake Ofisa wa Idara ya Fedha kutoka GGML, Gama Zephania Sogoni, ambaye ni mmoja wa wahitimu wa kike pekee mwaka huu alisema furaha ya kuhitimu inahitimisha safari ngumu yenye manufaa aliyopitia.

“Ilinibidi nifanye kazi za ziada kupanga ratiba yangu kwa sababu mbali na kazi, nilikuwa natakiwa kusoma na kulea ujauzito wangu lakini sasa ninajivunia mafanikio haya. Haikuwa rahisi,” alisema Gama.

GGML imebaki kuwa kampuni inayoongoza kwa ulipaji kodi bora katika tasnia ya uziduaji nchini baada ya kulipa zaidi ya Sh trilioni 3.9 kwa Serikali tangu kuanzishwa kwake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

error: Content is protected !!