Sunday , 5 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Hichilema kama Nyerere: Atinga Marekani na msafara wa watu 3, apiga teke ndege ya rais
KimataifaTangulizi

Hichilema kama Nyerere: Atinga Marekani na msafara wa watu 3, apiga teke ndege ya rais

Spread the love

 

ANAFUATA nyayo za Hayati Mwalimu Nyerere? Ndilo swali linaloibuka miongoni mwa Watanzania baada ya Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema kuelekea nchini Marekani kwa kutumia ndege abiria badala ya ndege binafsi ya rais huku akiwa ameambatana na msafara wa watu watatu pekee. Anaripoti Helena Mkonyi, TUDARCo … (endelea).

Hichilema amesafiri jana tarehe 19 Septemba kuelekea jijini New York kushiriki mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 Septemba 2021.

Neno moja kuu alilolitoa kuhusu safari yake, Hichilema ambaye amepanda ndege ya Shirika la Ndege la Qatar amesema mpangilio wa safari yake umelenga kubana matumizi.

“Tunakwenda New York kushiriki Mkutano Mkuu wa UN, tunakwenda kushirikiana na wadau mbalimbali na muhimu kwa faida ya nchi yetu. Tumekwenda ujumbe wa watu wachache ili kazi hii iwe na tija na gharama nafuu zaidi kwa taifa letu,” amesema.

Kauli hiyo imeibua mjadala katika mitandao ya kijamii huku baadhi ya wachangiaji wakimpongeza kwa hatua hiyo hasa ikizingatiwa nchi hiyo deni la zaidi ya Dola za Marekani bilioni 12.

Ikumbukwe kuwa Rais wa Kwanza na Baba wa Taifa Mwalimu, Julius Nyerere ni mmoja wa marais wanaoheshimika kwa kubana matumizi na kuacha kutapanya pesa.

Katika kipindi cha uongozi wake alikuwa anahudhuria mikutano ya aina hiyo kwa ndege za kawaida huku akiwa na msafara wa watu wachache.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

error: Content is protected !!