Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Mbowe: Shahidi wa pili amaliza kutoa ushahidi
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Mbowe: Shahidi wa pili amaliza kutoa ushahidi

Spread the love

 

SHAHIDI wa pili katika shauri dogo la kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, kwenye Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar ea Salaam, Inspekta Mahita Omari Mahita, amemaliza kutoa ushahidi wake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar ea Salaam … (endelea).

Inspekta Mahita aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha, amemamliza kutoa ushahidi huo leo Jumatatu, tarehe 20 Septemba 2021, mahakamani hapo mbele ya Jaji Mustapha Siyani.

Shauri hilo dogo lilitokana na mapinganizi ya mawakili wa utetezi, wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala, wakipinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili katika kesi ya msingi, Adam Kasekwa, yasitumike mahakamani hapo kama kielelezo na Kamanda Kingai, katika kesi ya msingi, wakidai yalichukuliwa nje ya muda kisheria.

Pia, katika mapingamizi hayo walihoji kwa nini mtuhumiwa alihojiwa Dar es Salaam, badala ya Moshi mkoani Kilimanjaro alikokamatwa.

Shahidi huyo wa jamhuri alianza kutoa ushahidi wake Ijumaa iliyopita, dhidi ya shauri hilo dogo, ambapo miongoni mwa mambo yaliyoibuka katika ushahidi wake ni chakula walichopewa watuhumiwa, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah.

Ling’wenya, mazingira ya mahojiano na namna watuhumiwa walivyosafirishwa kutoka Kilimanjaro hadi Dar ea Salaam.

Katika ushahidi wake, Inspekta Mahita aliongozwa na Mawakili wa Serikali Waandamizi, Robert Kidando akishirikiana na Pius Hilla.

Katika ushahidi wake, Inspekta Mahita alidai watuhumiwa walipewa chakula katika maeneo ya Bomang’ombe na Himo mkoani Kilimanjaro, wakiwa njiani kuelekea katika Kituo cha Polisi cha Kati cha Dar ea Salaam, kwa ajilo ya mahojiano.

Alitoa madai hayo baada ya mawakili wa utetezi, wakiongizwa na Peter Kibatala, kumuuliza swali kama watuhumiwa hao wawili walipatiwa chakula baada ya kukamatwa maeneo ya Rao mkoani Kilimanjaro na hadi walipofikishwa Dar es Salaam.

Inspekta Mahita pia aliieleza mahakama hiyo akidai, watuhumiwa hao walitimiziwa haki zao zote, wakati wanakamatwa na kuhojiwa, tofauti na madai ya upande wa utetezi ya kwamba watuhumiwa hao hawakutendewa haki, ukidai waliteswa na kuchukuliwa maelezo ya onyo pasina hiari yao.

Inspekta Mahita alianza kutoa ushahidi wake baada ya shahidi wa kwanza wa jamhuri katika shauri hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kinondoni, ACP Ramadhan Kingai, kuamliza kutoa ushahidi wake.

Katika shauri hilo dogo, jamhuri umepanga kuita mashahidi saba, ambapo wawili walishaitwa na sasa shahidi wa tatu anaendelea kutoa ushahidi wake.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!