Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Tangulizi Azam FC sasa kuvaana na pyramid ya Misri 
Tangulizi

Azam FC sasa kuvaana na pyramid ya Misri 

Spread the love

 

MARA baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya FC Horsed kutoka Somalia, klabu ya soka ya Azam FC, sasa itamenyana na Pyramid kutoka nchini Misri kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa kombe la Shirikisho barani Afrika. Anaripoti Hunda Mintanga TUDARCo … (endelea) 

Mchezo huo wa marejeano wa hatua ya awali ulipigwa leo, kwenye dimba la Azam Complex Chamazi, majira ya saa 10 jioni.

Ushindi huo utawafanya Azam FC, kuwa na jumla ya mabao 4-1, Kwenye michezo yote miwili ambayo walichezea kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Pyramid ambao itakuwa mara yao ya tatu kushuka nchini kwenye michezo ya kimataifa dhidi ya timu kutoka Tanzania.

Mara ya kwanza timu hiyo kuja nchini ilikuwa kwenye mchezo wa kimataifa ambao ulichezwa kwenye dimba la Ccm Kirumba tarehe 27 octoba 2019, dhidi ya Yanga na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Mara ya pili timu hiyo ilishuka nchini tarehe 17 Machi 2021, kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Namungo FC, nakuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Bao la Azam FC kwenye mchezo wa leo lilifunghwa na Ismael Kader dakika ya 38, kipindi cha kwanza na kuifanya timu hiyo kusonga mbele kwa hatua inayofuata.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Walimu 5000 Songwe waililia CWT kuwanyima sare

Spread the loveZaidi ya walimu 5000 ambao ni wanachama wa Chama cha...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

error: Content is protected !!