Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Walimu 5000 Songwe waililia CWT kuwanyima sare
Habari MchanganyikoTangulizi

Walimu 5000 Songwe waililia CWT kuwanyima sare

Spread the love

Zaidi ya walimu 5000 ambao ni wanachama wa Chama cha Walimu (CWT) mkoa wa Songwe, wameulalamikia uongozi wa chama hicho taifa kwa kushindwa kuwanunulia tisheti kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi) ambayo kimkoa yamefanyika wilayani Ileje. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe… (endelea).

Wakizungumza jana Jumatano wakati wa maadhimisho hayo, wanachama hao wamelalamika kutopatiwa fulana  ambazo ni sare ikilinganishwa na vyama vingine licha ya kwamba walikatwa fedha za kununua sare hizo.

Mwalimu wa Shule ya msingi Isansa wilaya ya Mbozi, Basilyusi Ngonela amesema hawakutegemea chama hicho kikubwa nchini katika maadhimisho makubwa kama hayo kushindwa kuwanunulia sare kama ilivyozoeleka na kusisitiza viongozi wa CWT kujitahimini.

“Walimu tunakatwa asilimia mbili kwenye mishahara yetu ambayo tulipaswa tununuliwe na tisheti kama sare ya sikukuu hii, lakini tukiwauliza viongozi wa mkoa wanasema tatizo ni makao makuu,” amesema Ngonela.

Bestina Mbuligwe ambaye naye mwalimu amesema wamesherekea sikukuu ya wafanyakazi kama yatima kwa kukosa sare kitendo ambacho kimepelekea kuzomewa na walimu wa chama kipya cha (CHAKUHAWATA).

“Kwa kweli viongozi wetu taifa hawajatutendea haki, inabidi watuambie shida nini,” amesema Mbuligwe.

Akizungumza kwa masharti ya kutoandikwa jina lake mmoja wa viongozi wa chama hicho mkoani humo amesema viongozi wa CWT taifa waliwaeleza kumekuwa na tatizo la usafirishaji tisheti hizo.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa huo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Daniel Chongolo ameeleza kusikitishwa na kitendo cha walimu ambao ni wana chama wa CWT.

Alisema kitendo cha wanchama hao kushindwa kuvaa sare kulikosababishwa na viongozi wao kushindwa kuwatimizia takwa lao kikatiba na kumewafedhehesha walimu hao kwenye sikukuu ya wafanyakazi.

“Kwa kweli hili jambo CWT hamjawatendea haki walimu na mkumbuke hili suala lipo kwenye mkataba ambapo kila wakati wa sikukuu ya wafanyakazi wanatakiwa wanunuliwe sare,” amesema Chongolo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!