January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Marekani kuwarejesha wahamiaji wa Haiti

Spread the love

 

SERIKALI ya Marekani chini ya utawala wa Rais Joe Biden inaendelea na mpango wake wa kuwarudisha nyumbani wahamiaji kutoka Haiti. Anaripoti Glory Massamu TUDARCo … (endelea).

Lengo ni kuzuia uhamiaji wa watu wengi katika kambi iliyopo Texas ambapo mpaka sasa takribani watu 14,000 tayari wamewasili.

Marekani inajiandaa kuwarudisha wahamiaji hao nchini Haiti kuanzia kesho Jumapili tarehe 19 Septemba 2021.

Wengi wa wahamiaji waliofurika chini ya daraja la barabara kuu, ni sehemu ya wimbi kubwa la wahamiaji wa Haiti, waliowasili kutoka Brazil, Chile na mataifa mengine ya Amerika Kusini, kutokana na tetemeko kubwa la ardhi, lililotoke nchini humo mwaka 2010.

Maafisa wa usalama wa ndani, wanapanga safari nane za ndege kuelekea Haiti huku mpango huo bado unajadiliwa na wanatarajia kutangaza safari hizo leo Jumamosi, amesema afisa mmoja wa Marekani.

Joe Biden, Rais wa Marekani

Serikali ya Haiti imekubaliana na mpango huo na kuomba angalau ziwe ndege tatu, lakini maafisa wa Marekani wanataka kuongeza idadi ya wahamiaji ili kupunguza kasi ya idadi kubwa ya watu katika kambi ya Del Rio huko Texas.

Amesema baadhi ya raia wa Haiti wanaotaka kuepuka kurudishwa nyumbani, wanaweza kujaribu kubaki Marekani kinyume cha sheria au kurejea Mexico, jambo ambalo haliruhusiwi ambapo wahamiaji hao wanaweka maisha yao hatarini.

Hata hivyo, watetezi wa wahamiaji wamekuwa wakimtaka Rais Biden kusitisha safari za kuwarudisha nyumbani kufuatia mauaji ya rais wa nchi hiyo, Jovenel Moise (53), yaliyotokea Julai 2021 na tetemeko la ardhi lililotokea Agosti 2021.

Rais Moise aliuawa tarehe 7 Julai 2021, katika shambulio akiwa katika makazi yake na watu ambao hawafahamiki.

Katika tetemeko hilo la ardhi lenye ukumbwa wa vipimo vya Ritcher 7.2 liliikumba nchi ya Haiti na kusababisha vifo vya takribani watu 304, kujeruhi 1,800 pamoja na kuharibu nyumba na miundombinu mbalimbali.

error: Content is protected !!