Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Michezo Kocha Simba: Tutacheza kwa heshima kubwa
Michezo

Kocha Simba: Tutacheza kwa heshima kubwa

Didier Gomes, Kocha wa Simba
Spread the love

 

KUELELEKEA kwenye tamasha la Simba maarufu kama ‘Simba Day’ kocha mkuu wa klabu hiyo, Didier Gomes amesema atacheza kwa heshima kubwa dhidi ya wapinzani wao TP Mazembe ambao watacheza mchezo wa kirafiki siku ya kesho. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Tamasha hilo litafanyika kesho 19 Septemba 2021, kuanzania Asubuhi kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo litamaliziwa na mchezo wa kirafiki kati ya Simba dhidi ya TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Congo.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelekea mchezo huo, kocha wa simba Didier Gomes amesema kuwa wanashukuru TP Mazembe kukubali mwaliko huo na watacheza kwa heshi a zote kutokana na ukubwa wa klabu hiyo.

“Itakuwa siku nzuri sababu tunaenda kukutana na mashabiki wetu baada ya muda kupita. Tunaishukuru TP Mazembe kwa kukubali kucheza na sisi Simba Day. Ni moja ya timu bora Afrika na tutacheza kwa heshima kubwa ili tushinde mchezo huu” Alisema Gomes

Simba wanaenda kufanya tamasha hilo kwa mwaka wa 13, ambapo litambatana na burudani mablimbali sambamba na kutambulisha kikosi chao kuelekea msimu ujao wa mashindano 2021/22.

Katika upande mwengine nahodha wa kikosi hiko John Bocco amesema kuwa, mchezo huo watatumia kama kipimo kuonesha walivyojiandaa kwa msimu mpya.

“Itakuwa ni mechi nzuri kwetu kujipima kwenda kuanza msimu. Kama wachezaji tupo tayari kuwaonesha tulivyojiandaa kwa msimu mpya. Tumejiandaa kuwafurahisha mashabiki wetu hivyo tunawaomba wajitokeze kwa wingi kuja kuona tulivyojipanga.” Alisema Bocco

1 Comment

  • Hello Kocha,
    Ni kipi kipya umeifundisha Simba?
    Haina mbinu za kushabulia, kujihami na kuwasoma wapinzani. Hii ndiyo sababu kubwa tunashindwa kushinda vizuri nyumbani.
    Timu inategemea uwezo wa mchezaji mmoja mmoja. Hii siyo mbinu.
    Tulipoifunga Azam bao moja ka kushinda mchezo ule, sikubaliani na goli hilo. Refa akipuliza kipenga kusimamisha mchezo kwa sababu ya adhabu, lazima wachezaji wasubiri kipenga cha kuanza tena mchezo, na siyo kuanza wakati refa anaongea na wachezaji wa Azam FC. Hii inaonyesha ushindi ni wa kuhonga. Mimi ningekuwa refa au TFF ningefuta hayo matokeo…inatia aibu timu kubwa zinalazimisha ushindi hazina mbinu. Hamtaifunga timu ya Nigeria…poleni kwa kurudisha nyuma soka la Tanzania.
    Namkumbuka marehemu Syler S. Mziray, alikuwa kocha mwenye mbinu. Alikwenda yanga na kushinda, akaja Simba na kushinda. Angeshinda na timu yeyote kwa sababu ana MBINU. Nitakuheshimu tukifika TAMU 16.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Ujanja ni kubeti na Meridianbet

Spread the love  JUMAPILI ya leo imekaa kihela hela sana ndani ya...

Michezo

Anza Jumamosi yako na mkwanja wa Meridianbet

Spread the loveJumamosi ya leo ODDS zimekaa kijanja sana ndani ya Meridianbet...

error: Content is protected !!