RAIA zaidi ya 20 wameuawa katika bonde la maajabu la Panjshir nchini Afghanistan katika mapigano baina ya Taliban na vikosi vya upinzani. Inaripoti Helena Mkonyi, TUDARCo kwa msaada wa Mitandao ya Kimataifa … (endelea)
Vyanzo vya habari vimeripoti, miongoni mwa waathirika wa tukio hilo ni muuzaji na baba wa watoto wawili Abdul Sami.
Wakati wa mapigano hayo, Sami hakutaka kuondoka katika eneo hilo la tukio huku akisema, yeye anamiliki duni na wala hana uhusiano wowote na mapigano hayo.
Lakini muuuzaji huyo, alikamatwa akituhumiwa kuuza kadi za simu kwa wapiganaji wa upinzani hali iliyosababisha kuuawa na mwili wake kutupwa karibu na nyumba yake.
Mashuhuda wa mwili huo walisema, mwili wa Sami ulionesha dalili zote za kuteswa kabla ya kifo chake.
Bonde hilo maarufu nchini humo la Panjshir, limekuwa kitovu cha upinzani Afghanistan chini ya kamanda wa upinzani Ahmad Shah Massoud, eneo hilo liliwafukuza vikosi vya Soviet na Taliban.
Bonde hilo limezungukwa na milima ambayo inawawia ngumu kwa wapinzani wanaojaribu kutaka kufika eneo hilo.
Ikumbukwe wakati Talibani walipoingia katika bonde hilo waliwahimiza wakazi wa eneo hilo kuendelea na shughuli zao za kawaida.
”Wanapaswa kutoka nje na kuendelea kufanya shughuli zao za kila siku,” alisema msemaji wa eneo hilo, Malavi Abdullah Rahamani.
Alisema kama ni wauzaji wanaweza kwenda kwenye maduka yao, ikiwa ni wakulima wanaweza kwenda kwenye mashamba yao, tuko hapa kuwalinda maisha yao na familia zao’.
Leave a comment