January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kimbunga chatikisa Texas, Louisiana

Spread the love

 

KIMBUNGA Nicholas kimetokea Texas nchini Marekani na kusababisha mvua kubwa, kuharibu miundobinu ya barabara na majengo. Anaripoti Glory Massamu, TUDARCo … (endelea).

Shule kadhaa katika majimbo ya Texas na Louisiana zimefungwa na mamia ya safari za ndege zimefutwa au kucheleweshwa katika viwanja vya ndege.

Kimbunga hicho kimetokea jana Jumatatu, tarehe 14 Septemba 2021 ambapo Rais wa Marekani, Joe Biden alitangaza hali ya dharura mjini Louisiana na kuamuru msaada kutolewa kwa maeneo yaliyoathirika.

Haya yanajiri wiki chache tu baada ya kimbunga Ida – ambacho ni cha tano kwa nguvu kuwahi kuikumba Marekani na kuwaacha zaidi ya wakaazi milioni moja wa Louisiana wakiwa hawana umeme.

Kituo cha Taifa cha Kimbunga cha Marekani kilionya athari za mafuriko ya kutishia maisha, hasa katika maeneo ya mji mkuu inaweza kutokea, hata hivyo Kituo cha Huduma ya Hali ya Hewa ya Taifa kilisema kuna hali ya kutishia maisha.

“Tunataka kuhakikisha kwamba hakuna mtu atayekutwa na dhoruba hii,” alisema Gavana wa Louisiana, John Edwards wakati akizungumza na waandishi wa habari

Kwa upande wake, Meya wa Houston, Sylvester Turner alionya juu ya mafuriko na kuwasisitiza wananchi wa jiji hilo kukaa mbali na barabara.

“Chukua vitu kwa umakini na ujiandae,” alisema Turner katika mkutano wa waandishi wa habari na kuongeza “hili ni tukio la mvua na hatujui ni mvua kiasi gani tutapata.”

error: Content is protected !!