Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema wamng’ang’ania IGP Sirro, watoa ujumbe
Habari za SiasaTangulizi

Chadema wamng’ang’ania IGP Sirro, watoa ujumbe

Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu Chadema Bara
Spread the love

 

CHAMA kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, kimewataka wadau mbalimbali wakiwemo vyama vya siasa, asasi za kiraia na vyombo vya habari kusimamia sheria za nchi ili zisivunjwe. Anaripoti Mwanaharusi Abdallah na Victoria Mwakisimba, TUDARCo … (endelea).

Pia, wamemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi nchini humo (IGP) Sirro Sirro kujiuzulu au kuondolewa kwenye wadhifa huo na mamlaka yake ya uteuzi.

Hayo yamesemwa leo Jumanne, tarehe 14 Septemba 2021 na Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Bara wakati anazungumza na waandishi wa habari, makao makuu ya chama hicho, Kinondoni mkoani Dar es Salaam, kuhusu kauli ya IGP Sirro aliyoitoa hivi karibuni.

Mara baada ya kurejea Tanzania kutoka katika ziara ya kikazi nchini Rwanda tarehe 10 Septemba 2021, IGP Sirro alisema katika ziara hiyo amejifunza namna jeshi la polisi la nchi hiyo linavyokabiliana na vitendo vya ugaidi na kuahidi kufanyia kazi mikakati yao hapa nchini ili kudhibiti vitendo hivyo.

“Tumeona wenzetu shule za dini, madrasa na sunday school kuna kikosi malaum kinapitia kuona mafunzo yanayotolewa je ni ya kizalendo au kuharibu nchi.”

“Tumeona ni uzoefu mzuri na sisi tushirikishe viongozi wa dini na timu ya kupambana na makosa ya ugaidi namna gani tupitie mafunzo ya kwenye dini shuleni hadi vyuo tuone mafunzo yanayotolewa ni kwa ajili ya kuwajenga au kuwabomoa vinana wa kitanzania,” alisema IGP Sirro.

Kutokana na kauli hiyo, Kigaila amesema, IGP Sirro anataka kuleta utaratibu ambao ni kinyume cha taratibu na kanuni za katiba ya nchi ambao ni kutembelea taasisi za kidini na kuangalia kama mafunzo yanayo tolewa ni ya uzalendo.

Amesema, anachokitangaza IGP Sirro kinakwenda kinyume cha katiba na sharia “kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 19 katika kuenzi dini au kuendesha ibada majukumu hayo yatafanywa nje ya mamlaka.”

“Anachokifanya IGP Sirro ni ukikwaji wa katiba, tunatoa wito kwa taasisi za habari, vyama vya siasa, Watanzania, asasi za kiraina na taasisi za dini kuhakikisha wanailinda katiba na sheria ili isivunjwe.”

“Tusimame kwa pamoja kuitaka mamlaka ya uteuzi kumwondoa madarakani IGP Sirro kwani anachokifanya au anachotaka kufanya ni kuvunja katiba na sheria kitu ambacho kimekatazwa kwa kila mmoja wetu,” amesema Kigaila.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!